Mji wa Musoma na viunga vyake vyote umelazimika kusimama kwa muda kupisha mkutanop mkubwa wa kampeni nuliokuwa ukiongozwa na mgombea urais kwa tiketi ya Chadema anayeungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Mh.Edwrad Lowassa,
Hatimaye ameivunja rekodi mjini Musoma.
Ilikuwa ni siku iliyoulazimu mji huu wa Musoma kusitisha kudhughuli zake huku barabara zikipigwa deki kwa ajili ya Edwrad Lowassa.
Katika siku yake ya pili ya kampeni akitumia chopa alimehutubia mikutano mikubwa sita tofauti iliyohudhuliwa na idadi kubwa zaidi wananchi huku akiahidi kuboresha miundombinu ya maji, afya, elimu, kuukarabati uwanja wa ndege wa mji huo, ikiwa ni pamoja na kufufua matumani ya ujenzi wa chuo kikuu ndani ya mji wa Musoma.
Fredrick Sumaye waziri mkuu mstaafu licha ya kutoa ya kutosha ya namna watanzania wanavyoweza kumpa ushindi Edward Lowassa, amesema siri kubwa ya maendeleo ya Tanzania ni kukinyofoa madarakani chama cha CCM.
No comments:
Post a Comment