Kwenye list ya Wanasiasa walioamua kuingia kwenye Mchakato wa Uchaguzi Mkuu Tanzania utakaofanyika October 2015, alikuwepo pia Mwanasiasa Mkongwe, MchungajiChristopher Mtikila ambaye alitangaza kugombea nafasi ya Urais kupitia Chama chaDemocratic Party (DP).
October 04 2015 taarifa zimetufikia kuhusu msiba wake, Mchungaji Mtikila amefariki baada ya kupata ajali ya gari ndogo eneo la Chalinze akiwa na watu wengine watatu ambao wamepata majeraha.
Tayari ninazo picha kutoka Mikocheni Dar es Salaam, nyumbani kwa MarehemuMchungaji Mtikila.. ndugu, jamaa na watu wengine wameanza kukusanyika kwa ajili ya kuendelea na taratibu nyingine za Msiba.
Taratibu za Msiba mpaka hatua ya mazishi zote nitakuwa nakusogezea kila zinaponifikia… #RIPMchungaji MTIKILA.
PICHA KWA HISANI YA MILLARDAYO.COM
No comments:
Post a Comment