Na Walter Mguluchuma
Waumini wa Kanisa la Kiijili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Ziwa Tanganyika inayounda Mikoa ya Katavi na Rukwa imepanga kufanya ibada ya misa Oktoba 24 badala ya Oktoba 25 ilikuwapa nafasi waumini wa Kanisa hilo kushiriki uchaguzi mkuu utakao fanyika Jumapili ya oktoba 25
Hayo yalisemwa hapo jana na Askofu wa KKT Dayosisi ya Ziwa Tanganyika wakati alipokuwa akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu wakati akiwa Sumbawanga Mkoa wa Rukwa
Alisema Kanisa limeamua kuhamishia ibada hiyo siku ya juma mosi badala ya jumapili ili kutowa nafasi kwa waumuni wa Kanisa hilo kushiriki kakamilifu uchaguzi mkuu wa Oktoba 25
Kanisa linatambua umuhimu wa uchaguzi Mkuu ndio maana limehamisha shughuli zake zote ambazo zilikuwa zifanyike jumapili ya Oktoba 25 na badala yake zitafanyika jumamosi ya oktoba 24
Nae Katibu wa Dayosisi hiyo Abrahamu Kombe amesema kuwa Kanisa limefanya jambo zuri sana kuhamishia ibada siku hiyo ya jumamosi badala ya jumapili
Alisema hakuna tena muumini wa Kanisa hilo Katika Dayosisi ya Ziwa Tanganyika ambae atashindwa kupiga kura kwa kisingizio cha kuwa alikuwa kwenye ibada
Mpaka saa kuna baadhi ya Madhehebu ya Dini mbalimbali hapa nchini wameishatangaza kuhamishia ibada zao siku ya jumamosi ya tarehe 24 badala ya tarehe 25 oktoba kwa ajiri ya kupisha uchaguzi mkuu utakaofanyika siku hiyo wa kuwachagua Wabunge na Madiwani na Rais
No comments:
Post a Comment