Saturday 31 October 2015

JUST IN....NDEGE YA URUSI YENYE WATU 224 YAANGUKA SINAI, MISRI

Ndege ya Shirika la Kogalymavia la Urusi, Airbus A-321 iliyoanguka eneo la Sinai nchini Misri.

Egyptian prime minister Sharif Ismail, pictured, has formed an emergency committee to deal with the crash
Waziri Mkuu wa Misri, Sharif Ismail akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Ramani ikionyesha eneo la Sinai nchini Misri ilipotokea ajali hiyo.
NDEGE ya Shirika la Kogalymavia la Urusi, iliyowabeba abiria 200, watoto 17 na wafanyakazi wa ndege hiyo 7, imeanguka katika eneo la Sinai nchini Misri, ofisi ya waziri mkuu wa Misri imethibitisha.
Ndege hiyo aina ya Airbus A-321 ilikuwa imetoka Mji wa Sharm el-Sheikh ikielekea mji wa St. Petersburg nchini Urusi ilipoanguka.
Vyombo vya habari nchini Misri vinasema mabaki ya ndege hiyo yamepatikana na magari 50 ya kubebea wagonjwa yametumwa eneo la ajali.
Awali, kulikuwepo na utata kuhusu hatima ya ndege hiyo, baadhi ya ripoti zikisema ilitoweka karibu na Visiwa vya Cyprus. Lakini ofisi ya Waziri Mkuu wa Misri, Sharif Ismail amethibitisha kwamba ndege hiyo ilianguka katikati ya eneo la Sinai.
Waziri Mkuu wa Misri, lsmail ameunda kamati ya dharura ya kushughulikia ajali hiyo.
Shirika la Urusi linalosimamia safari za ndege, Rosaviatsiya limesema ndege hiyo iliyokuwa katika safari nambari 7K 9268 iliondoka Sharm el-Sheikh saa 06:51 saa za Moscow (0:351 GMT) na ilitarajiwa kuwasili Uwanja wa Ndege wa Pulkovo mjini St Petersburg saa 12:10 leo.
Ndege hiyo ilikosa kuwasiliana na wasimamizi wa safari za ndege Cyprus dakika 23 baada ya kupaa kama ilivyoratibiwa na ikatoweka kutoka kwenye mitambo ya rada.
Kituo maalum kimefunguliwa Uwanja wa Ndege wa Pulkovo kusaidia abiria waliokuwa kwenye ndege hiyo, shirika la habari la Tass limesema likinukuu maafisa wa Jiji la St Petersburg

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!