Mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa chama cha kisiasa cha DP Christopher Mtikilaamefariki dunia alfajiri ya leo wakati akitokea Morogoro kuelekea Dar es salaam.
Taarifa zilizotufikia kupitia kwa kamanda wa Polisi Pwani Jafari Mohamed amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na alifarika saa 12 kasorobo katika kijiji cha Msolwa, Chalinze akiwa kwenye gari ndogo huku wenzake watatu wakijeruhiwa vibaya.
Mtikila alitangaza kugombea Urais kupitia chama chake cha DP lakini chama chake ni moja ya vyama ambavyo vilikatwa na NEC kutokana na kutotimiza baadhi ya masharti na vigezo vilivyomo kwenye fomu ya Mgombea Urais.
Tutaendelea kukuletea taarifa zaidi.
Mara ya mwisho camera ya AyoTV kumnasa Mchungaji Mtikila ilikua Aug 2015 kwenye headlines za kuchukua fomu kwenye tume ya taifa ya uchaguzi.
No comments:
Post a Comment