Leo katika Fainali za Bongo Star Search (BSS) Season 8, 2015 Juma Kayumba ameibuka Mshindi
- Amejinyakulia kitita cha jumla ya shilingi milioni 50, fedha za Kitanzania
Ikiwa leo ni fainali ya mashindano haya. Washiriki wapo 6, anahitajika mshindi mmoja atakayeibuka na kitita cha shilingi milioni 50 Usiku huu.
==============
Mchuano umeanza, ushindani mkali sana .
Wapo washiriki sita, wanahitajika watano waweze kuingia top 5.
Kila mshiriki ataimba wimbo mmoja ili mchujo upite wabakie watano.=================
- Waimbaji wote sita mpaka sasa wameshaimba nyimbo mojamoja. Majaji wanachuja majina sita yapatikane matano.
- Kampuni ya Huawei kupitia wawakilishi wake wanagawa zawadi ya simu kwa washiriki wote sita.
TOP 5:
- Wafuatao wamechaguliwa kuingia 5 bora;
1.Kayumba Juma
2.Angel Merikato
3.Nasib Fenabo
4.Frida Amani
5.Kevin.
- Mshiriki aliyeshindwa kufuzu ni Jackline, anatoka katika mashindano.
No comments:
Post a Comment