Thursday, 22 October 2015

JESHI LA POLISI KUIMARISHA ULINZI SIKU YA KUPIGA KURA

  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akionyesha waandishi wa habari leo (hawapo pichani) kitabu cha maadili ya uchaguzi kilichosainiwa na viongozi wa vyama vya siasa waliosimamisha wagombea katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25.


 
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akionyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) kitabu cha maadili ya uchaguzi kilichosainiwa na viongozi wa vyama vya siasa waliosimamisha wagombea katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 ambapo amewataka watu wote kutii sheria bila shuruti wakati wa uchaguzi.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akifafan jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)
Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo Mkuu wa Jeshi hilo IGP Ernest Mangu amesema kuwa ulinzi utaimarishwa maeneo yote kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha kuwa taifa linapita salama katika kipindi hiki cha kupiga kura, kuhesabu na kutangaza matokeo ya uchaguzi.

Ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kupiga kura siku hiyo bila wasiwasi wa aina yoyote ili kuweza kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi.
(Picha na Francis Dande)

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!