Mama mjamzito anatakiwa kuandaa bag lake atakalo kwenda nalo hospital kujifungulia pale muda unapokaribia wiki ya 36-40 .Unatakiwa kufanya maandalizi mapema sababu unaweza patwa na uchungu kabla ya siku za makadirio.Unatakiwa uplan hospital utakayo jifungulia kabla ya kujifungua inakuwa rahisi kwako na ni vizuri uchague ya karibu ila yenye huduma nzuri.
List ya mahitaji yanakuwa ni yako na ya mtoto ,
1:Khanga au vitenge pair 2-3
2.Chupi za size kubwa sio za kukubana pair 4-5
3.Maternity pads zinauzwa pharmacy 5000TSHS
4:Breast pads /nursing pads (kuzia maziwa yasivuje)
5:Bras/brazia za kuvaa pair 2 za kunyonyeshea au za kawaida
6.Nguo zako za kubadili 2-3 kwa wale wanao penda madera au magauni mapana mapana yanafaa.
7.Slippers/ kandambili
8:Chanuo kama ukiwa ujasuka
9.Body lotion yako
10:Dawa ya mswaki na mswaki
11:Tochi kwa wale wanaishi maeno ya kukatika umeme
12:Taulo ndogo ndogo unaweza tumia wewe na mtoto pair 3
13.Simu yako na chaji
14:Camera au video camera kwa wale watakao jifungulia wanaweza chukua kumbu kumbu yako.
15:Lip balm kupaka mdomo usikauke hata ukija tembelewa unaona aibu
16.Deodorant (kupaka makwapani) usafi bado muhimu
Mahitaji ya mtoto
17:Nguo zake pair 5-10
18.Diaper /nepi pair
19:Mfuta yake
20:Kitana
21:Nail cutter(kukatia kucha)
22.Soksi pair 2-3
23.Kofia yake
24:Kiblanket chake kumfunikia akilala au akibebwa
25.Baby wipes
26.Sweta 1-2
kwa wale watakao jifungulia private hospitals kunaa baadhi ya vitu hutakiwi kwenda navyo ,ila kwa wale wanaojifungulia hospital za selikalini wanatakiwa kubeba kama
1:Ndoo ya kuwekea nguo chafu
2:Pamba,viwembe,
3.Cloves
SHUKRANI KWA AFYA BORA YA MTOTO.
No comments:
Post a Comment