Majeneza yenye miili ya marehemu yakiandaliwa kwa kuagwa.
Rais Dk Jakaya Mrisho Kikwete na mgombea Urais wa tiketi ya CCM Dk John Pimbe Magufuli wakitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza ya aliyekuwa Mbunge wa Ludewa(CCM) Marehemu Deo Filikunjombe na wenzake wawili waliofariki katika ajali ya helikopta juzi katika pori la akiba la mbuga ya Selous. Marehemu aliagwa katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam, asubuhi ya leo.
Rais wa Jamhuri ya Dk Jakaya Mrisho Kikwete na mgombea Urais wa tiketi ya CCM Dk John Pimbe Magufuli wakitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza ya aliyekuwa Mbunge wa Ludewa(CCM) Marehemu Deo Filikunjombe na wenzake wawili waliofariki katika ajali ya helikopta juzi katika pori la akiba la mbuga ya Selous. Marehemu aliagwa katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam, asubuhi ya leo.
Rais wa Jamhuri ya Dk Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa mke wa marehemu Deo Filikunjombe, Sarah Filikunjombe.
Rais wa Jamhuri ya Dk Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa mke wa marehemu Deo Filikunjombe, Sarah Filikunjombe.
Ndugu, jamaa na marafiki wakipita kwenye majeneza yenye miili ya marehemu kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Deo Filikunjombe likitolewa ndani na kuwekwa eneo maalum kwa ajili ya kuagwa nyumbani kwake, Mtoni Kijichi, Dar.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Egdi Francis Mkwera likitolewa ndani na kuwekwa eneo maalum kwa ajili ya kuagwa nyumbani kwa Filikunjombe, Mtoni Kijichi, Dar.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Plasdius Ngabuma Haule likitolewa ndani na kuwekwa eneo maalum kwa ajili ya kuagwa nyumbani kwa Filikunjombe, Mtoni Kijichi, Dar.
Waombolezaji wakionekana wenye huzuni, simanzi na majonzi
Mke wa marehemu Deo Filikunjombe, Sarah Filikunjombe akisaidiwa kwenda kuaga mwili wa marehemu mme wake.
Mke wa marehemu Deo Filikunjombe, Sarah Filikunjombe akisaidiwa kwenda kuaga mwili wa marehemu mme wake.
Miili ya marehemu watatu kati ya wanne waliokufa kwenye ajali ya chopa (helikopta) iliyotokea usiku wa kuamkia jana, Oktoba 16, 2015 katika Hifadhi ya Selous, eneo la Msolwa mkoani Morogoro, imeagwa leo jinini Dar es Salaam.
Shughuli ya kuaga miili ya marehemu hao ilianzia katika hospitali ya Lugalo ambapo rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete aliwaongoza mamia ya Watanzania kuaga miili ya marehemu hao ambao ni aliyekuwa Mbunge wa jimbo la ludewa, Mhe. Deo Filikunjombe (43), Plasdius Ngabuma Haule na Egdi Francis Mkwera aliyetajwa kuwa Ofisa Tawala wa Wilaya ya Tarime.
Baadhi ya viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo waziri Mkuu anayemaliza muda wake, Mizengo Pinda, Spika wa Bunge Anne Makinda, Mgombea urais kwa tiketi ya CCM ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, Dk John Pombe Magufuli, ndugu, jamaa na marafiki.
Baada ya kumaliza kuaga hapo Lugalo, miili ya marehemu ilipelekwa nyumbani kwa Deo Filikunjombe maeneo ya Mtoni Kijichi jijini Dar, kwa ajili ya kuagwa ndugu na majirani. Zoezi hilo lilitanguliwa na ibada fupi ya kuombea miili ya marehemu hao kabla ya kuagwa na kusafirishwa kwa ndege kwenda nyumbani kwao Ludewa Njombe kwa mazishi.
PICHA NA DENIS MTIMA/GPL
No comments:
Post a Comment