Lazaro Nyarandu
Mama mjane wa marehemu akiweka taji la maua katika Nyumba ya milele ya Mumewe Deo Filikunjombe
Spika wa bunge akizungumza na waandishi wa habari baada ya Mazishi katika Makaburi ya Kanisa Katori mjini Ludewa
Spika wa Bunge la Tanzania Anna Makinda akiweka taji la maua katika Kaburi la Deo Filikunjombe leo,
Zito Zubery Kabwe akiweka taji la maua katika kaburi la Rafiki yake mpendwa Deo Filikunjombe, leo jioni
SPIKA wa bunge la jamuhuri ya Tanzania Anna Makinda amesema kuwa Mbenge marehemu Deo Filikunjombe, alikuwa ni mbunge wa tofauti kutokana na alivyo kuwa akiyanyakazi zake na alikuwa hakaibungele alikuwa anapenda kukaa na wananchi.
aAizungumza na waandishi wa habari Spika Makinda alisema kuwa Filikunjombe alikuwa ni mbunge wa tofauti na alipenda kuwa na wananchi mda wote na kila alipokuwa akimaliza bunge alikuwa anakimbilia kwa wananchi wake.
Alisema kuwa alikuwa ni mpiganaji kwa kufanya kile anacho kiamini serikali inaenda tofauti kukipigia kelele na huhakikisha wananchi wanapata haki zao.
Alisema kuwa wananchi wamempoteza mpigania haki zao na wakakikishe kuwa wanaangalia mbunge atakeye kuwa tayari kumalizea mipango yao aliyo kuwa ameianza mbunge wao.
"Filikunjombe alikuwa ni mbunge jasili na alikuwa akiwatetea wanaLudewa na watanzania kwa ujumla yeye alikuwa anawapenda sana wananchi wake, alikuwa anapenda wakaribu na wananchi, yeye jioni akimaliza bunge analudi kwa wananchi, ukimpigia simu asubuhi kama ulikuwanaye jioni atakwambia nipo jimboni," Alisema Makinda.
Aliongeza kwa kutoa wito wa watu wanao litaka jimbo la Ludewa kuhakikisha kuwa wanakuja kutekeleza yale aliyo kuwa ameyaanza Deo na kukamilisha mipango yake huku akisema kuwa mbunge hiyo alikuwa na mipango ya miaka mingi kuifanya Ludewa ya tofauti.
Alisema kuwa Deo alikuwa ni mbunge mweye kupenda maendeleo na kuleta umeme katika jimbo hilo pamoja na barabara za kufika katika maeneo mbali mbali ya jimbo hilo.
Aidha wa upande wake Rafiki yake mpendwa Wa Fili kunjombe, Kiongozi mkuu wa chama cha ACT wazalendo, Zito Kabwe, amesema kuwa anasikitika kutokea kwa msiba wa rafiki yake mpendwa na kuwa hatoweza kumpata rafiki wa aina ya Filikunjombe kutokan ana alivyo kuwa.
Alisema kuwa kwa wakazi wa Ludewa wamempoteza mtu muhimu sana na kuwa hawata kuja kumpata mbunge kama huyo licha ya kuwa watapata mbunge lakini kufanana na Deo ni Vigumu,
“Nasikitika kumpoteza rafiki yangu mpendwa nitapata marafiki lakini sio kama Deo, na hata kwa wakati wa Jimbo la Ludewa ni vigumu kumpata mbunge mweye hadhi ya Deo kwa kuwa alikuwa ni Mbunge mweye hamu ya kutetea wakazi wa jimbo lake na wakazi wengine,” alisema Kabwe.
Aliongeza kuwa Deo kwa kuwa aliwapenda wana Ludewa wakati ajali inatokea alijaribu kuruka na mwili wake ulikutwa mbali kidogo na mabaki ya ndeke inaonekana alikuwa anataka kujiokoa na kuungua na moto uliokuwa ukiwaka kutoka ilipo angukia Ndege.
Akihubiri katika ibada ya mwisho ya msiba wa marehemu hao watatu ambao ibada ilikuwa ni moja Askofi wa Kanisa la Romani Katoliki jimbo la Njombe, ask. Alfred Maluma alisema kuwa msiba huo ni mkubwa kwa kuwa umehusisha watu watatu wanao tokea sehemu moja na kuwatia moyo wafiwa kwa kuwaambia kuwa wawe wavumilivu katika siku hizi ngumu kutokana na msiba wenyewe ulivyotokea na ughafla wake.
Akielezea safari ya kuja kutoka Mjini Njombe kuelekea wilayani Ludewa alisema kuwa walikuwa wakisimamishwa kila mahali na wananchi wakilia kuonyesha masikitiko yao juu ya kifi ya Filikunjombe.
Alisema kifo chake kimewashitua wengi kutokana na alivyo kuwa akiwasaidia wananchi na kuwa wananchi katika vijiji mbalimbali walikuwa wakilia kwa sauti licha ya kupita Usiku katika maeneo hayo.
Mwili wa marehemu uliwasili usiku majira ya saa 7usiku katika mji wa Njombe baad ya kufanya ibada katika kanisa katiliki Njombe mjini na kuaza safari kuingia nyumbani kwao mjini Ludewa ibada za kumuaka Marehemu Deo Filikunjo,mbe na wenzake Egid Nkwera, Casablanka Haule ambao walikuwa wakisafiri kwa pamoja kutoka jijini Dar Es salaam kuja mkoani Njombe.
Msiba huo ambao umekuwa mkubwa kwa wakazi wa Jimbo la Ludewa ulio kusanya umati mkubwa wa wakazi wa Ludewa na watu kutoka sehemu mbalimbali maduka katika mji wa Ludewa yalifungwa kwa siku mzima huku wakazi wa mji huo wakiomboleza msiba wa mbunge wao.
Katika msiba huo kuna kuna viongozi mbalimbali waliofika kuomboleza akiwemo Mkuu wa mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi, Waziri wa maliasili na Utalii Lazaro Nyarandu, Wiliamu Lukuvi, na viongozi wengine wa chama cha mapinduzi wa nyazifa mbalimbali.
Aidha kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Wilayani Ludewa wamesema kuwa hawata mpata mmbunge mweye aina ya mbunge wao na kuwa Msiba huo kwa kuwa umetokea kwa ghafla wamesikitika sana ni bora angeumwa wangejua anaumwa.
Naye mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga na mgombea wa ubunge jimbo la Makambako alisema kuwa Jumapili iliyo pita alikuwa katika jimbo hilo kupiga kampeni kumsaidia marehemu anasikitika kutokea kwa msiba huo, huku akibubujikwa na machozi alisema kuwa alipiga kampeni katika vituo saba na kuwa aliagwa kuwa mgomba huyo jumanne iliyo pita alimuaga kuwa anaenda Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment