Friday, 2 October 2015

ALIYEUA WATU 77 NCHINI NORWAY ATISHIA KUSUSIA CHAKULAHADI AFE

Breivik
Image captionBreivik anatumikia kifungo cha miaka 21 gerezani
Mwanamume aliyeua watu 77 nchini Norway ametishia kususia chakula hadi afe, akilalamika kwamba anateswa gerezani.


Vyombo vya habari vinasema Anders Behring Breivik anadai kutengwa kutoka kwa wafungwa wengine tangu Septemba 2, na kwamba huwa anaruhusiwa kutoka nje ya seli yake saa moja tu kwa siku.
Breivik aliua watu 77 kwamba 2011 alipolipua bomu katikati mwa Oslo kabla ya kufyatulia risasi mamia ya vijana waliokuwa wamekusanyika katika kisiwa cha Utoya nchini humo.
Alihukumiwa kifungo cha miaka 21 jela 2012.
Madai hayo yake kwamba anawekwa katika hali mbaya ameyatoa kwenye barua aliyoandika na kuituma kwa vyumba vya habari Norway na Sweden.
Kwenye barua yake, Breivik, 36, anasema hali ngumu gerezani imemlazimisha kuacha kozi yake ya sayansi ya siasa aliyokuwa akisoma katika Chuo Kikuu cha Oslo.
"Kusoma na kufanya mawasiliano ni jambo lisilowezekana chini ya mazingira kama haya,” alisema kwenye barua.
Breivik alisema hali ikisalia ilivyo, atasusia chakula hadi afariki dunia, kwa mujibu wa vyombo vya habari Norway.
Mkurugenzi wa gereza la Skien anakozuiliwa Breivik, Ole Kristoffer Borhaug, aliambia BBC kwa sasa hakuna mtu anayesusia chakula gerezani humo.
Waziri wa Haki wa Norway Anders Anundsen alikataa kuzungumzia madai hayo ya Breivik, kwa mujibu wa gazeti la Dagbladet.
BBC

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!