Sunday, 20 September 2015

MAGUFULI ATAJA WIZARA TATU ATAKAZOHANGAIKA NAZO ZAIDI

Mgombea urais kupitia CCM Dk John Magufuli akihutubia wananchi wa mji wa Lamadi mkoani Simiyu kwenye mkutano wa kampeni za CCM. (Picha na Adam Mzee).

MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Mapinduzi, ameanza kuweka hadharani mawaziri watakaopata shida katika uongozi wake, kutokana na kazi zitakazokuwa mbele yao.


Akizungumza katika mikutano midogo na mikubwa wakati akitokea Simiyu kwenda mkoani Tabora jana, Dk Magufuli ambaye amekuwa akipita katika barabara zisizo za lami, alisema mawaziri hao watapaswa kufanya kazi usiku na mchana.
“Baraza langu la mawaziri, litakuwa la watu waadilifu, wachapa kazi na walio tayari kutumikia Watanzania,” alisema jana na kuongeza kuwa yeye alikuwa akitumwa, sasa anaomba kazi ili akawatume mawaziri hao.
Wizara za shida Tangu alipoanza kampeni, Dk Magufuli amekuwa akiweka wazi kuwa Waziri atakayerithi ofisi yake ya Wizara ya Ujenzi, atatakiwa kufanya kazi kuliko alivyofanya yeye na ikibidi alale katika maeneo yanayojengwa barabara.
Dk Magufuli katika uongozi wake wa miaka 15 katika wizara hiyo, amesimamia ujenzi wa barabara zenye urefu wa zaidi ya kilometa 17,000, wakati wakoloni waliokaa tangu miaka ya 1884 na 1885 mpaka 1961, waliacha mtandao wa barabara za lami wenye urefu wa kilometa 1,360 tu.
Waziri mwingine ambaye ameweka wazi kuwa atapaswa kujitathmini kama ataweza jukumu hilo, la sivyo ajiondoe mapema baada ya kumteua endapo atachaguliwa kuwa rais ni wa wizara itakayobeba jukumu la afya.
Wizara hiyo kwa mujibu wa Dk Magufuli, itapaswa kuhakikisha dawa hazikosekani katika hospitali zote za umma, kuanzia zahanati katika mitaa na vijiji, vituo vya afya katika kila kata, hospitali za wilaya na hospitali za rufaa katika kila mkoa.
Dk Magufuli ameahidi wananchi kuwa katika uongozi wake, itakuwa mwiko kusikia mgonjwa baada ya kumuona daktari, ametumwa kwenda kununua dawa katika maduka. Kuhusu kero ya maji, Dk Magufuli alisema kama akiwa Waziri wa Ujenzi alijenga zaidi ya kilometa 17,000 za lami, wakati kilometa moja ya lami ni zaidi ya Sh bilioni 1.5, hatashindwa kujenga mabwawa ya maji na mtandao wa mabomba ya kusambaza maji kwa wananchi.
Alikumbusha tena kuwa Waziri atakayeteuliwa kushika wizara hiyo, ajiandae kwa kuwa akishindwa ataondolewa mara moja. Pamba, mifugo Akiwa katika Jimbo la Kishapu, Dk Magufuli alizungumzia zao la pamba na mifugo na kuwadokeza wananchi kuwa yeye alisomeshwa kwa kutumia zao la pamba.
Alisema anajua zao hilo limepungua bei kutokana na udhaifu uliopo katika vyama vya ushirika na kazi atakayofanya ili kuongeza bei hiyo, ni kujenga viwanda vya nguo vitakavyotumia pamba hiyo, badala ya kuuza marobota ya pamba nje yakatengeneze nguo zitakazouzwa nje.
Kuhusu mifugo, alisema Serikali yake inataka kuhakikisha Tanzania inaachana na uuzaji wa mifugo hai, badala yake iwe na viwanda vya nyama ili kutoka maeneo ya wafugaji, viwanda vya nyama viuze nyama iliyokwishawekwa katika vihifadhio.
Akifafanua namna atakavyojenga viwanda, Dk Magufuli alisema Tanzania imepata rasilimali ya gesi asilia, ambayo inatoa malighafi ya kutosha na itatoa nishati ya kutosha kuwezesha ujenzi wa viwanda hivyo.
Wachimbaji wadogo Akiwa njiani kwenda Kishapu, katika eneo la Maganzo kwenye eneo la wachimbaji wadogo, Dk Magufuli alisema atahakikisha maeneo ya wachimbaji wakubwa yanapotengwa, yatengwe sambamba na maeneo ya wachimbaji wadogo.
Ahadi nyingine Dk Magufuli katika mikutano hiyo, amekuwa akiahidi kushusha bei ya vifaa vya ujenzi hasa saruji, mabati na misumari, ili wananchi wanaofanya kazi wajenge nyumba bora.
Katika kuongeza idadi ya Watanzania wanaofanya kazi ili kufikia lengo hilo, Dk Magufuli alisema katika kila mtaa na kijiji, Serikali yake itatoa Sh milioni 50 kwa ajili ya kuanzisha na kukuza biashara ndogo za wanawake na vijana.
Alisema atataka kila anayefanya kazi apate kipato kizuri kitakachomsaidia kukabiliana na mahitaji ya maisha yake, ikiwemo kujenga nyumba bora kutokana na kushushwa kwa bei za bidhaa za ujenzi.
Mbali na kutoa mikopo hiyo izunguke katika ngazi ya kijiji na mtaa, Dk Magufuli pia alisema Serikali yake itazuia kila aina ya usumbufu unaofanywa kwa wafanyabiashara hao, ikiwemo kukamatwa kwa bodaboda na mama ntilie.
Aidha aliahidi kuondoa ushuru unaosumbua wafanyabiashara wadogo na hasa wakulima, ili wafanye biashara kwa uhuru wajipatie kipato halali. Katika elimu, amekuwa akiahidi kuhakikisha kuanzia mwakani, wanafunzi kutoka darasa la awali mpaka kidato cha nne, wanasoma bila kulipa ada, ili kuondolea wazazi usumbufu wa watoto wao kurudishwa nyumbani kwa kukosa ada.
Kwa wanafunzi wa elimu ya juu, amewahakikishia kuwa hakutakuwa na usumbufu wa kupata mikopo na kuwataka wanaohusika na kazi hiyo, kuwa tayari kwa kuwa atataka kila mwenye

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!