Kampuni ya kuuza nguo za kifahari ya H&M imetumia picha za mwanamitindo wa kwanza Muislamu aliyevalia hijab(vazi la kiislamu linalostiri nywele na kichwa cha mwanamke).
Mariah Idrissi, mwenye umri wa miaka 23, mkaazi wa London Uingereza ndiye mwanamke wa kwanza kupata fursa hiyo ya kuwa kwenye jarida la maduka hayo yenye asili ya Sweden.
Mariah ni mmoja tu kati ya wanamitindo wapya waliosajiliwa chini ya nembo mpya ya maduka hayo 'Close the Loop'.
Talanta yake ilitambuliwa na mmoja wa watayarishaji wa maonyesho katika kampuni ya maonyesho.
Mmoja wa marafiki wake anasema kuwa alipomfahamisha kuwa alikuwa amepewa fursa ya kuonyesha mavazi ya H&M
Bi Maria alishtuka na kumuliza iwapo walijua kuwa yeye hujifunga Hijab (vazi la kiislamu linalostiri nywele na kichwa cha mwanamke)
''je wanajua kuwa mimi ninajifunga Hijab ?'' Aliuliza Maria.
Mariah -anamiliki duka la mapambo ya wanawake 'salon' inayouza henna na mapambo mengine ya kucha ambayo ni halali kwa mujibu wa dini ya kiislamu.
'Si jambo la kawaida kwa duka la kifahari kama hilo kutumia picha ya mwanamke aliyejistiri kwa hijab katika matangazo yake ya kibiashara.'' Alisema Mariah
'kwa hakika ni ni jambo la kujivunia sana kujumuishwa katika kampeini yao mpya ya matangazo ya kibiashara' Maria alinukuliwa na jarida la BuzzFeed.
''Nafikiri kuwa ni jambo la busara kuwatumia wanawake wa Kiislamu kwenye matangazo ya kibiashara kwa sababu Islam ndio dini ya pili kwa ukubwa duniani''Alisema Mariah.
Mariah sasa anasema anatazamia kuwaona 'wanawake waliojistiri katika maonyesho makubwa' zaidi ya fashoni duniani.
No comments:
Post a Comment