Wednesday, 5 August 2015

WAKIMBIZI WA SOMALIA WAREJESHWA MAKWAO

Wakimbizi wa Somalia warejesha kwao
Wakimbizi wa kwanza 100 wamerejeshwa Somalia kufuatia makubaliano kati ya Shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia maswala ya wakimbizi,UNHCR na serikali ya Kenya na Somalia.


Uhamisho huo wa kujitolea wa wakimbizi umeafikiwa baada ya Kenya kutishia kuwafurusha wakimbizi wa Somalia baada ya mashambulizi ya kigaidi yaliyotekelezwa na kundi la wapiganaji kutoka Somalia al Shaabab.
Awali Kenya ilikuwa inawasafirisha wakimbizi kwa mabasi lakini kutokana na changamoto za kiusalama katika eneo la Kaskazini Mashriki mwa Kenya ,UNHCR imeanzisha safari za moja kwa moja kutoka Daadab kwenda Somalia.
Uhamisho huo unafuatia mazungumzo baina ya Kenya Somalia na UNHCR
Kiongozi wa UNHCR bwana Raouf Mazou anasema kuwa ''huu ni mwanzo mpya''
''Ndege za kwanza mbili, zimeondoka Daadab kuelekea Kismaayona miji mingine midogo ya Luuq na Baidoa.''
Serikali ya Kenya ilikuwa imetishia kuwafurusha wakimbizi wa Somalia kutoka kwenye kambi ya Dadaab kufuatia ripoti za kijasusi zilizoeleza kuwa njama zote za mashambulizi ya Kundi la wapiganaji wa Kiislamu kutoka Somalia,Al Shabaab yalikuwa yakipangwa na kufanikishwa kutoka Dadaab.
Kenya ilitoa amri hiyo punde baada ya wanamgambo wa kiislamu wa Al Shabaab kuwaua wanafunzi wakristu takriban 150 katika chuo kikuu cha Garissa mapema mwezi Aprili.
Kenya ilikuwa inatishia kuwafurusha wakimbizi kufuatia mashambulizi ya Al Shabaab
Kambi hiyo yenye wakimbizi takriban nusu milioni ndio kubwa zaidi duniani ikiwa na asilimia kubwa ya wakimbizi kutoka Somalia.
Serikali ya Kenya imesema inaushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa asilimia kubwa ya mashambulizi yanayotekelezwa nchini Kenya na kundi la waislamu la Al Shabaab yanapangiwa katika kambi hiyo ya Dadaab.
Haswa ikiashiria shambulizi la maduka ya kifahari ya Westgate ambapo ilidawia washambulizi waliingia nchini kama wakimbizi.
Kambi hiyo yenye wakimbizi takriban nusu milioni ndio kubwa zaidi duniani
UNHCR inapinga madai hayo.
UNHCR inasema kuwa Kenya itakuwa inakiuka wajibu wake wa kuhakikishia wakimbizi usalama wao pindi wapoingia katika mipaka yake.
Serikali ya Kenya kwa ushirikiano na UNHCR na serikali ya Somali iliweka mipango ya kurejesha wakimbizi makwao mwaka uliopita lakini mkataba huo ulikuwa utekelezwe kwa hiari.
Idadi ndogo sana ya wakimbizi hao walikubali kurejea makwao kwa hiari.
BBC.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!