Hili ni ️tatizo la kawaida kwa wamama wajawazito kupungukiwa damu mwilini kipindi cha ujauzito !hii inatokana na mwili kuhitaji damu nyingi kwa ajili ya ukuaji wa ️mtoto,tatizo hujitokeza kipindi cha miezi mitatu ya mwisho (third trimester).
upungufu wa damu kwa mama ️ mjamzito upo wa aina 3 tofauti
Iron -deficiency anemia-ni upungufu wa madini ya chuma- ambao una sababisha kuzalisha kiwango kidogo sana cha damu.
Folate -deficiency anemia. Mama anakuwa na upungufu wa damu unaotokana na kukosa folic acid mwilini ambayo inasaidia Kwenye utengenezaji mpya wa cells na uzalishwaji wa red blood cells ,mama aliekosa folic acid anaweza kuzaa mtoto mwenye mapufungu kama kuzaliwa mgongo wazi au kichwa kikubwa hivyo mama anatakiwa kumeza vidonge vya folic acid kipindi cha miezi 3 ya mwanzo mwamimba.
VitaminsB12 deficiency anemia- mama anakuwa na ukosefu wa vitamini b12 inayohitajika kwenye uzalishaji wa chembe hai nyekundu(red blood cell) .Mlo wa mama unapokuwa sio kamilifu unaweka hitilafu ya kuzalishwa kwa chembe nyekundu na kuadhiri uzalishwaji wa damu ,mama anatakiwa kula nyama,kuku,maziwa na mayai ili kusaidia kuzalishwa kwa damu mwilini.
Dalili kwa upungufu wa damu mwilini
Kusikia kizungu zungu
Kukosa nguvu
Kubadilika rangi ya mwili kuwa mweupe kuliko kawaida , utaona viganjani,kwenye kucha ,macho na ulimi
Kukosa umakini wa kuona vizuri
Mapigo ya moyo Kwenda mbio
kushindwa kupumua vizuri
Kuvimba miguu
Adhari za upungufu wa damu kwa mama mjamzito
mama mjamzito anakuwa na hatari kubwa ya kupoteza uhai wake pindi ajifunguapo,sababu zoezi zima la kujifungu linahitaji damu ya kutosha ,akipoteza damu nyingi ni hatari kwake kuishiwa damu mwilini. Upungufu wa damu kwa mama humwadhiri mtoto tumboni na
Kuzaliwa mwenye afya dhoofu alie na uzito mdogo.
Mtoto kuzaliwa kabla ya mda Wake(njiti)
Mtoto kuwa na upungufu wa damu
Mtoto kuzaliwa kiwa amechoka (fetal distress)
Mtoto ukuaji Wake unadumaa ,stage za ukuaji unakuwa mbaya na kuadhiri maendeleo duni ya kiakili.
Wamama wenye hatari ya kupata tatizo la upungufu wa damu (anemia)
Wenye kushika mimba zaidi ya mtoto mmoja (mapacha)
Mimba za utotoni
Wenye matatizo ya upungufu wa damu kabla ya kushika mimba
Kushika mimba kwa haraka baada ya kujifungua mtoto mwingine
Wanao kula lishe isijitosheleza kwenye madini ya chuma
Tiba
Upungufu wa damu unaweza tibika kwa haraka na kuokoa maisha ya mama na mtoto ,kinachotakiwa mama anahitaji kupima kiasi cha damu kila ahudhuriapo klinik.Na anaweza kuongeza damu kwa kutumia vidonge vya madini ya chuma kwa miligram 2-4.8 kwa siku.
Kutumia vidonge (supplements) za folic acid zinasaidia kuongeza kiasi cha damu kwa haraka
Tumia matunda ya beetroot unaweza yachemsha ukatengeneza juice , unanweza ukasaga ukanywa au ukapikia kwenye chakula zinapatikana masoko ya kisutu aua kariakoo sokoni kwa bei kati ya 3000-5000 Tshs hapo.
Kula matunda kwa wingi, tafuna au kunywa juice ya nyanya
Tumia juice ya rosella glasi 2-3 kwa siku
Kula mboga za majani spinach,mchicha,brocoli au matembele kwa wingi
Kula dagaa au kunywa supu ya maharagwe kwa wingi
Kula nyama,kuku na samaki
kunywa maziwa ,cheese na kula mayai
Ushauri toka kwa afyabora kwa mtoto.
Zingatia kupima kiasi cha damu mara kwa mara uendapo klinik, ni hatari kupungukiwa na damu hata kama ni kiasi kidogo kipindi chote cha ujauzito.
CHANZO: AFYABORA KWA MTOTO
No comments:
Post a Comment