Infection ya masikio ni tatizo kubwa kwa watoto,sikio limejigawa sehemu kuu 3 ya ndani ,nje na kati. Matatizo mara nyingi yana shambulia sehemu ya kati(Otitis media) inashambulia watoto wachanga na watoto wadogo na nyingine ni sehemu ya ndani (Otitis externa) hii inawashambulia sana wale wanao ogelea mara kwa mara na pia linajitokeza kipindi sana cha baridi.
Inakuwa ngumu mzazi kujua chanzo chake,kuna baadhi ya wazazi wanadharau kutatilia tiba yake,mwishowe masikio ya mtoto hutoa usaha mzito na harufu kali na kumpelekea kuwa na tatizo la kutokusikia vizuri.
Hili tatizo linawashambulia sana watoto walio chini yamwaka 1 kwa asilimia 50%,watoto walio na Miaka 3 na kuendelea kwa 70% na kwa Watu wazima ni kwa 30%! Husababishwa na bacteria au virus wanaoshambulia Kwenye ngoma ya sikio!
Kuna sababu tofauti zinazo changia mtoto kupata infection ya sikio baada ya bacteria kushambulia ,kwawazazi wanaovuta sigara wanachochea kwa 37% ya kushambuliwa na infection ya sikio kwa urahisi.Mzingo(allergies) mtoto anapopata allergy inaweza kwenda kublock eustachian tubes ambazo zinaungana na pua,koo na sikio la kati ,kufungwa kwa tubes hizo husababisha kutengeneza maji maji masikioni yanayokuja mletea infection.Upungufu wa kinga mwilini unachangi mtoto kupata infection.
Dalili ya mtoto mwenye infection ya sikio
Kupata homa
Kukosa hamu ya kula.
kuhara na kutapika kwa wingi!
kukosa raha na kulia sana kutokana na maumivu makali.
kusugua au kuvuta vuta sikio lake .
Sikio kutoa usaa wa njano au mweupe wenye harufu kali
kushindwa kulala !
kuvimba sikio na macho kuwa mekundu.
kushindwa kusikia vizuri .
Adhari ya kupata infection ya masikio
mtoto anatakiwa kupata tiba kwa haraka akiwa amepata infection ya masikio sababu inamletea madhara makubwa kama
Kuwa kiziwi-mtoto anashindwa kusikia vizuri .
Uti wa mgongo-mtoto anapata tatizo la uti wa mgongo baada ya bakteria kushambuliautandu (membrane) inayofunika ubongo na uti wa mgongo.
Kushambuliwa kwa ngoma ya sikio
Mtoto kuchelewa kuongea.
Tiba
Mpeleka mtoto haraka hospital iwapo utakapo ona ana dalili hizo ,haswa watoto wengi wanaanza kwa kuharisha na kutapika!
Antibiotics – mtoto atapewa ,ingawa kwa watoto walio chini ya miezi 6 hawashauri kupewa antibiotics kuna dawa zao nyingine iwapo haikumtibu basi atapewa.
Maziwa ya mama ,watoto wengi wasio nyonyesha chini ya miezi Sita wanahatari ya kushambuliwa na bacteria !(Maziwa ya mama ni kinga kubwa kwa mtoto mnyonyeshe mpaka miaka 2)
Mtoto atapimwa kama anaweza kusikia vizuri
Watatumia kifaa cha Otoscope -kinachoingizwa sikioni .
Atachukuliwa kipimo cha CT SCAN itakayo fanyiwa kichwani
Zingatia
Mwoshe mikono mtoto mara kwa mara
Kwa wale wanaowapa watoto plastik ya nyonyoa(pacifier) usimpe mpaka apone!
Unapomwogesha mtoto hakikisha maji yasimwingie masikioni iwapo yakaingi hakikisha unamtowa ,na msafishe masikio mara kwa mara kila aogapo kwa kutumia cotton pads.
Watoto wengine wanaweza kupatwa na infection ya sikio zaidi ya mara moja kinachotakiwa mzazi umpe dose yote alioandikiwa na daktari.
CRD: Afya bora kwa mtoto.
No comments:
Post a Comment