Muhubiri Mkuu wa Sherehe za Makambi mtaa wa Manzese Mch. Idelphonce Tirumanywa akihutubia watu waliohudhuria sherehe hizo. Ujumbe Mkuu "Mtizame Yesu Ukaishi"
Kwaya Maalum ya Jangwani kutoka Shinyanga ikitumbuiza wakati wa Sherehe za Makambi ya Mtaa wa Kanisa la Waadventista Wasabato Manzese
Kikosi maalum cha vijana wadogo wa Kanisa la Waadventista Wasabato Manzese (Wavumbuzi) wakitembea kwa mwendo wa gwaride kuelekea jukwaani kwa ajili ya program maalum kwenye sherehe za makambi
Watoto wa Mtaa wa Manzese wakionesha program maalum jukwaani kwenye sherehe maalum za makambi ya Manzese
Mch. Amos Lutebekela (Kushoto) akimkabidhi zawadi ya shukrani mkufunzi wa vijana Bw. Chris Buhatwa wakati wa kuhitimisha sherehe za Makambi mtaa wa Manzese
Baaadhi ya washiriki wa sherehe za makambi wakisikiliza kwa makini vipindi vinavyoendelea kwenye Makambi ya Mtaa wa Manzese
Baadhi ya wabatizwa wakipokelewa na wachungaji na wazee wakanisa wakati wa kuhitimisha sherehe za makambi
Mch. Idelphonce Tirumanywa akinyoosha mkono juu kuomba wakati wa kufanya huduma maalum ya ubatizo kwa watu walioamua kujiunga na kanisa la waadventista wasabato ulimwenguni.
Kwaya ya Angaza ikimwimbia Mungu siku ya kuhitimisha sherehe za makambi Manzese
Sherehe za Makambi kwa mwaka 2015 katika Mtaa wa Manzese zimemalizika kwa kishindo cha kubatiza waumini ishirini na saba (27) ambao wameamua kumpokea Yesu kwa kujiunga na kanisa la Waadventista Wasabato Manzese.
Akizungumza na waumini wa kanisa hilo wakati wa kuhitimisha sherehe hizo mwishoni mwa wiki, Mchungaji Idelphonce Tirumanywa amesisitiza kuwa kanisa kuendelea kuwalea vyema waumini wapya waliojiunga na kanisa hilo. Mch. Tirumanywa pia ameendelea kuwaasa waumini wote wa kanisa la waadventista wasabato kuwa mfano bora kwa jamii kwa kuonesha matendo mema yatakayo warudisha watoto wa Mungu waliopotea nyumbani.
“Ni wakati wakurudi nyumbani, dunia ipo kwenye hatari kubwa, tena kubwa sana. Tunapoishukuru serikali yetu kwa uhuru wa kuabudu, waadventista wasabato wote amkeni muumtangaze Mungu ili watoto wa Mungu waache dhambi na kurudi nyumbani”, alisistiza Mch. Tirumanywa.
Sherehe za makambi ya mtaa wa Manzese yalihudumiwa na kwaya maalum kutoka Sauti ya Jangwani Shinyanga wakishirikiana na kwaya tatu (3) zinazounda mtaa huo yaani Angaza, Mbiu na Sauti ya Nyikani zote kutoka Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA SARAH REUBEN
No comments:
Post a Comment