Sunday, 16 August 2015

SAKATA LA MADAKTARII FEKI" CHAMA CHA MADAKTARI KUSAJIRI UPYA



Ili kukabiliana na  wimbi la ‘madaktari feki’, Chama cha Madaktari (MAT) pamoja na  Baraza la Madaktari wa Tanganyika, watasajili upya wanataaluma hao ili watambulike na kufuatiliwa kwa urahisi.



Wakati taasisi hizo zinajipanga kufanya kazi hiyo, mapema wiki hii mganga feki ambaye ni mkazi wa Katesh mkoani Manyara, Mohammed Abdallah,  alinaswa baada ya kutibu  wagonjwa zaidi ya 20 licha ya kwamba hana cheti wala uzoefu wa  taaluma hiyo.

Tukio hilo ni mfululizo wa kukamata madaktari feki likitanguliwa na mengine mengi yaliyotokea  katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Mifupa (Moi), Hospitali ya Rufaa ya Dodoma  wakihujumu afya za watu na taaluma hiyo kwa kutoa matibabu wakati si madaktari.

Akizungumzia kuhusu kushamiri kwa matukio ya aina hiyo, Rais mstaafu wa chama hicho, Dk. Prinus Saidia, alisema watu hao wamekuwa wakiidhalilisha taaluma hiyo na kwamba vyombo vya dola vinapowakamata vinatakiwa kuwaadhibu.

Alisema licha ya juhudi za kuwanasa  kufanyika lakini wanapofikishwa kwenye taasisi za kisheria huachiwa na baadaye kuendeleza utapeli wao.

“Mfano yupo aliyekamatwa Muhimbili lakini baadaye aliachiwa huru. Hii inatuvunja moyo na kuwapa nguvu watuhumiwa  kuendeleza matukio haya,” alisema.

Alisema MAT imeliona tatizo  hilo na kwamba kuanzia  mwaka jana wameanza utaratibu wa  kuwatambua madaktari walipo kwa kuwasajili ili kujua idadi kwa  nchi nzima.

Alisema mchakato huo unapofanyika unarudisha jina la daktari kwenye kitabu alichosajiliwa ili  kuwezesha kujua ngazi na kiwango cha  taaluma zao na idadi yao pia.

Kadhalika aliiomba serikali kuhakikisha kuwa, wale wanaotoa tiba mbadala na kutumia jina la  daktari wanapigwe marufuku, ili kuwapa heshima madaktari waliosomea taaluma hiyo

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!