Friday, 28 August 2015

MH: MWAKYEMBE AZUNGUMZIA SAKATA LA RICHMOND MBEYA

Aliyekuwa mwenyekiti wakamati teule ya bunge ya kuchunguza kashfa ya mkataba tata wa Richmond iliyomuondoa madarakani aliyekuwa waziri mkuu Mh Edward Lowassa, Mh Harrsion Mwakyembe amewahakikishia watanzania kuwa walijiridhisha pasipo shaka kuhusika kwa Edward Lowassa katika sakata la Richmond na kwamba hawakumsingizia kama anavyojitetea hivi sasa.



Huyo ni Mh Harrison Mwakyembe aliyekuwa mwenyekiti wa kamati teule ya bunge ya kuchunguza kashfa ya Richmond iliyomwondoa madarakani aliyekuwa waziri mkuu wa kwanza wa serikali ya awamu ya tatu ambaye kwa sasa ni mgombea wa kiti cha urais kupitia  umoja wa vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA kwa tiketi ya Chadema Mh Edward Lowassa wakati akitoa ufafanuzi kwa wananchi wa Kyela mkoani Mbeya kuhusiana na sakata hilo kwamba Mh Lowassa hakusingiziwa na kutahadharisha kuwa kesi ya jinai haina ukomo.
 
Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Mh Mwigulu Lameck Nchemba amewatahadharisha watanzania kutopeleka viongozi aliowaita wasaka dili ikulu kwa kuwa majuto ni mjukuu. 
 
Katika mojawapo ya mikutano ya hadhara iliyofanyika mkoani Mbeya hii leo katika wilaya ya Rungwe baadhi ya wanachama wa vyama vya upinzani wamerejesha kadi za vyama vyao kikiwemo Chadema na kujiunga na CCM kwa madai ya kuchoshwa na siasa za kutumikishwa kwa ajili ya viongozi wa juu wa chama hicho.
 
Mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi Dr John Pombe Magufuli ambaye hii leo hakuwa katika ubora wake kutokana na sauti yake kutotoka vyema amewataka watanzania kumpa kura za ndio ili Tanzania iweze kupaa kimendeleo.
 
Ziara ya Dr Magufuli kusaka ridhaa ya watanzania kwa ajili ya kumpa mamlaka ya kuliongoza taifa kupitia sanduku la kura inaendelea ambapo jumamosi ya August 29 anatarajiwa kuzungumza na watanzania wa mkoa wa Njombe.

ITV.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!