Friday, 28 August 2015

MCHINA KORTINI AKIDAIWA KUKUTWA NA MENO YA SIMBA JIJINI DAR


RAIA wa China, Jianfeng Wu amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka ya kukutwa na meno ya simba yenye thamani ya Sh milioni 10.1.


Baada ya kusomewa mashitaka, mshitakiwa hakuruhusiwa kujibu mashitaka kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo ya uhujumu uchumi isipokuwa Mahakama Kuu.
Awali, wakili wa Serikali, Paul Kadushi alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha kuwa ilikuwa Agosti 18, mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Wu alipokamatwa akiwa na meno matatu ya simba. Hakimu Mkeha aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 10, mwaka huu itakapokuja tena mahakamani hapo kwa hatua nyingine.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!