Friday, 14 August 2015

MAUAJI STAKISHARI WENGINE WATATU MBARONI


JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limewashikilia watu watatu wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya askari, raia, kujeruhi, kupora silaha Kituo cha Polisi Sitakishari, kilichopo Ukonga, Dar es Salaam.



Kamanda wa kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema kukamatwa kwa watuhumiwa hao, kunafanya idadi yao kufika  wanane kati ya hao, watatu walifariki dunia baada ya kurushiana risasi na polisi katika harakati za kuwakamata.

Aliongeza kuwa, jeshi hilo linaendelea na operesheni ya kuwasaka watuhumiwa wengine wakishirikiana na polisi wa Mikoa ya Pwani, Tanga ikidaiwa katika mikoa hiyo kuna kambi za wahalifu.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Zahaq Ngai (35), kwa jina maarufu 'Mtu Mzima', mkazi wa Tuangoma na ndiye kinara wa genge lililofanya tukio hilo na kusababisha vifo vya watu saba, kupora silaha kadhaa.

Mwingine ni Ramadhani Hamis (18) 'Luatule', mkazi wa Mandimkongo na Omary Amiri (24), mkazi wa Mbagala, Dar es Salaam ambao wote wanaendelea kuhojiwa ili kupata taarifa ambazo zitafanikisha  kukamatwa kwa mtandao wote.

"Bado tunaendelea kuwasaka watuhumiwa, ahadi ya sh. milioni 50 iliyotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, iko palepale kwa atakayefanikisha kukamatwa kwao.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!