Tuesday, 11 August 2015

MAGUFULI AAGIZA WATU WANAFUNZI NA WATU WENYE ULEMAVU WASAFIRI BURE


Serikali imeagiza wanafunzi na watu wenye ulemavu katika Manispaa ya Mtwara Mikindani na kata ya Msangamkuu, watasafiri bure kwenye kivuko cha Mv Mafanikio.

 
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli,  wakati akimkaribisha Rais Jakaya Kikwete kuzindua kivuko hicho.
 
Alisema wanafunzi wote waliovaa sare za shule hawatatozwa nauli kutokana na kundi hilo kuwa tegemezi.
 
“Walemavu na wanafunzi watavuka bure bila kutozwa hata shilingi 10, ili mradi tu awe amevaa sare za shule na walemavu pia hawatatozwa pesa yoyote na kwa wengine ni lazima tuendelee kuchangia mafuta ili kivuko hiki kitusaidie na kuwa endelevu,” alisema.
 
Magufuli alisema kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba abiria 100 pamoja na magari kimegharimu Sh. milioni 3.3, fedha kutoka serikalini. 
Akihutubia wananchi wa Msangamkuu pamoja na Mtwara wakati wa uzinduzi huo,  Rais Jakaya Kikwete alisema serikali imetatua kero hiyo ya kivuko iliyokuwa ikiwakabili wananchi kwa muda mrefu.
“Kupatikana kwa kivuko hiki ni fursa nzuri kwenu kitumieni kwa kuuza bidhaa mbalimbali, kama mkazi wa Msangamkuu una ming’oko yako unahitaji kwenda kuuza mjini tumia kivuko hiki kwa maendeleo yenu” alisema Rais Kikwete.
Alisema  kutokana na wakazi wa maeneo hayo kukosa kivuko tangu kupatikana kwa uhuru, watu wengi walipoteza maisha na kuwataka kukitumia kivuko hicho  vizuri.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!