Saturday, 29 August 2015

EU KUTUMA WAANGALIZI 128 WA UCHAGUZI TANZANIA

UMOJA wa Ulaya (EU) utatuma timu ya waangalizi yenye wajumbe 128 nchi nzima kwa ajili ya kushiriki katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25, 2015.


Hayo yalibainishwa wakati wa uwekaji saini wa makubaliano ya awali ya kuruhusu timu hiyo kuja nchini kulikofanywa jana baina ya EU na Serikali ya Tanzania katika Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Uwekaji saini huo umefanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula kwa niaba ya serikali na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Filiberto Ceriani Sebregondi kwa niaba ya EU.
Akizungumza baada ya uwekaji saini wa makubaliano hayo, Balozi Sebregondi alisema kuwa EU imekuwa ikituma timu hiyo kwa nchi washirika ambazo zina historia nzuri ya demokrasia na kwamba nchi hizo zina dhamira ya dhati ya kukuza mahusiano na EU kwa kuruhusu waangalizi wafanye majukumu yao katika hatua zote za uchaguzi kwa madhumuni ya kuhakikisha kuwa uchaguzi unakuwa wa haki na huru

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!