Msanii wa kizazi kipya na mkali wa miondoko ya R&B Ben
Pol akitumbuiza katika jukwaa la Coke Studio wakati wa tamasha la Coke Studio
Afrika msimu wa tatu lililofanyika mwishoni mwa wiki nchini Kenya.
Wasanii wengine walikuwepo katika tamasha hilo ni Wangechi (Kenya) pamoja na Silver Stone (Ghana)
Wasanii wengine walikuwepo katika tamasha hilo ni Wangechi (Kenya) pamoja na Silver Stone (Ghana)
Msanii wa kizazi kipya na mkali wa miondoko ya R&B Ben
Pol kutoka nchini (kulia) na Wangechi kutoka Kenya wakitumbuiza katika jukwaa
la Coke Studio wakati wa tamasha la Coke Studio Afrika msimu wa tatu
lililofanyika mwishoni mwa wiki nchini Kenya.
Msanii wa kizazi kipya na mkali wa miondoko ya R&B Ben
Pol kutoka nchini (kushoto) na Wangechi kutoka Kenya wakitumbuiza katika jukwaa
la Coke Studio wakati wa tamasha la Coke Studio Afrika msimu wa tatu
lililofanyika mwishoni mwa wiki nchini Kenya.
Msanii maarufu wa miondoko ya Hiphop kutoka nchini Kenya
Wangechi akitumbuiza katika jukwaa la Coke Studio wakati wa tamasha la Coke
Studio Afrika lililofanyika mwishoni mwa wiki nchini Kenya
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Wangechi (Kenya), Ben Pol
(Tanzania) na Silva Stone (Ghana) walitumbuiza katika jukwaa la Coke Studio
wakati wa tamasha la Coke Studio Afrika lilofanyika nchini Kenya mwishoni mwa
wiki.
Na mwandishi wetu.
Msimu wa tatu Coke Studio Afrika umeanza ambapo
ilishuhudiwa
wasanii Ben Paul kutoka Tanzania na Wangechi (Kenya) na Silver Stone
(Ghana) wakitumbuiza katika jukwaa la Coke Studio na kuamsha nderemo na vifijo
kwa mashabiki ambao walihudhuria tamasha hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki
hii nchini Kenya.
Nyimbo iliyoonekana kukonga nyoyo za mashabiki katika tamasha hilo ni ile ya ‘Sophia’ ambayo
aliimba kwa kushirikiana na Wangechi, ambapo inataja moja kwa moja mji wa
Dodoma, ambao ndio makao makuu ya hapa nchini.
Msimu huu wa Coke Studio umeambatana na kampeni mpya yenye
jina la ‘Sababu Bilioni za Kuamini’, na hivyo kujumuisha vijana mbalimbali
ambao wanaamini katika kufikia malengo yao bila ya kujali changamoto
zinazowakabili.
Katika tamasha hilo kulikuwa na vijana watano kutoka
Tanzania wenye vipaji mbalimbali ambao walipata fursa ya kujifunza kupitia
mambo mbalimbali baada ya kueleza namna wanavyojiamini katika kutimiza ndoto
zao.
Vijana hao ni Minaeli Benedict, Stanley Meshack Mafundo,
Hassani Singizi, Jackson, Shabani Swaibu (wote kutoka Dar es Salaam) na Jackson
Kassian (Morogoro).
Baada ya kumalizika kwa tamasha hilo, vijana hao walipata
fursa ya kuzungumza na wasanii hao ambao pia ni vijana kabisa, na kuelezwa
mbinu ambazo zitawawezesha kupambana na hatimaye kufikia ndoto zao.
Katika kuhakikisha vijana hao hawakati tamaa kufikia malengo
yao, Ben Pol aliwaambia kwamba, mpaka kufikia mafanikio aliyonayo sasa,
amepitia changamoto nyingi sana ikiwemo kunyimwa nafasi ya kurekodi nyimbo zake
na waandaaji mbalimbali wakiamini kuwa hakuwa na uwezo wa kuimba lakini licha
ya kufanyiwa hivyo aliendelea kupambana mpaka kufanikiwa kufika alipo sasa.
“Ninachotaka kuwaambia ni kwamba, mfano, kwa wale wenye vipaji
vya kuimba, kitu kikubwa unachotakiwa kufanya ni kuwa na nyimbo nyingi ambazo,
hata ukirekodi moja isipofanya vizuri, unatoa nyingine ili kuhakikisha
unaendelea kusikia masikioni kwa watu”, alisema
“Kitu kingine ni kwamba unaposimama mbele ya watu, waone ni wa kawaida tu na wala usiwagope, bila
ya kujali nyadhifa zao isipokuwa kikubwa ni kutowaonesha dharau”, alisisitiza.
Wangechi kwa upande wake alisema : “ Vijana wa jinsia zote
ni muhimu kujiamini na kuondokana na dhana kwamba jinsia fulani ndio wanaweza
kitu fulani, kwa mfano mimi naweza kufanya ‘hiphop’ na R&B, sasa wasichana
wengi hata kama wanaweza, huogopa kufanya Hiphop wakiamini kwamba ni mziki wa
kiume lakini kumbe yeyote anaweza kuimba”.
Lengo kuu la Coke Studio Afrika ni kuwakutanisha kwa pamoja
wasanii wenye mbalimbali wa Afrika na kuimba nyimbo ambazo zina vionjo tofauti
hivyo kuongeza msisimuko. Lakini vilevile kutoa fursa kwa wasanii wachanga kushirikiana na wakubwa ili kuwapa changamoto
ya kuongeza ujuzi katika kazi zao na kuzidi kukuza vipaji vyao
Katika msimu huu wa Coke Studio Afrika, ni wasanii kutoka
mataifa matano tu tu ndio wamechaguliwa
kutumbuiza. Mataifa hayo ni Nigeria, Msumbiji, Kenya, Uganda na Tanzania.
No comments:
Post a Comment