Picha ya pamoja ya Mgombea urais, Mh. Edward Lowassa, Mgombea Mwenza Haji Duni, Mgombea Urais Zanzibar Maalim Seif, Wenyeviti wenza wa UKAWA, Mhe Freeman Mbowe, Mh. James Mbatia, Dk. Emmanuel Makaidi pamoja na viongozi waambatanishi.
Mgana Msindai aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Singida CCM akikabidhiwa kadi ya Chadema na Mhe. Mbowe.
Makongoro Mahanga aliyekuwa Waziri wa Ajira na Kazi pia ni Mbunge wa Segerea naye akikabidhiwa kadi ya Chadema kutoka kwa Mbowe.
Mbunge wa Arumeri Magharibi Ole Medeye naye akipokea kadi yake ya Chadema.
Isaya Simon Bukakiye aliyekuwa Katibu wa Uchumi na Fedha Wilaya ya Kahama CCM naye akipokea kadi yake ya Chadema.
Washiriki wa mkutano huo wakiimba Wimbo wa Taifa.
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mhe. Freeman Mbowe akihutubia.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zanzibar, Salum akiongea na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema.
Mke wa Mhe. Lowassa, Regina Lowassa akiingia katika Mkutano Mkuu akifuatana na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA), Mhe. Halima Mdee.
Mke wa Mhe. Lowassa, Regina Lowassa akiingia katika Mkutano Mkuu akifuatana na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA), Mhe. Halima Mdee.
VIGOGO wanne waliokuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hatimaye leo wamejiunga rasmi na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kukabidhiwa kadi zao za uanachama kutoka kwa Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Mhe. Freeman Mbowe.
Zoezi hilo limefanyika leo wakati wa Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Vigogo hao ni pamoja na Mgana Msindai aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Singida CCM, Makongoro Mahanga aliyekuwa Waziri wa Ajira na Kazi pia ni Mbunge wa Segerea, Mbunge wa Arumeri Magharibi Ole Medeye na Isaya Simon Bukakiye aliyekuwa Katibu wa Uchumi na Fedha Wilaya ya Kahama CCM.
Mbali na usajili huo, Juma Duni Haji ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) ngazi ya Taifa na Waziri wa Afya wa Serikali ya Zanzibar naye amejiunga rasmi na Chadema ambapo pia amechaguliwa kuwa mgombea mwenza wa Waziri Mkuu wa zamani, Mhe. Edward Lowassa katika nafasi ya urais ndani ya chama hicho.
Katika mkutano huo, Mhe. Lowassa ametangazwa rasmi kuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema huku Juma Duni Haji akitangazwa kuwa mgombea mwenza.
Aidha Chadema wamewapendekeza wagombea hao kupatiwa nafasi na vyama vingine vinavyounda Ukawa ili viwapitishe wawe wagombea wao wa urais kwa tiketi ya Ukawa
No comments:
Post a Comment