Jeshi la Chad linasema kuwa limewauwa zaidi ya wanamgambo 100 wa Boko Haram katika kipindi cha majuma mawili yaliyopita.
Wanamgambo hao wanasemekana waliuwawa katika makabiliano makali katika visiwa vilivyoko kwenye ziwa Chad.
Aidha taarifa hizo bado hazijathibitishwa.
Kundi la wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram, lilianzia Kaskazini Mashariki mwa Nigeria,lakini sasa wanaendesha mapigano katika mataifa kadhaa magharibi mwa Afrika.
Alhamisi iliyopita,bunge la Chad lilipitisha sheria iliyoruhusu kunyongwa kwa watu watakaopatikana na hatia ya kushiriki ugaidi.
Hata hivyo wanaharakati wa kupigania haki za kibinadamu nchini humo wanasema kuwa sheria hiyo itatumiwa kuwakandamiza watu.
BBC
No comments:
Post a Comment