Butternut squash ni jamii ya maboga ila hili linavirutubisho zaidi na ndio mana madaktari wengi wa watoto wanashauri mtoto apewe butternut squash akifika miezi sita muda sahihi wa mtoto kuanza kujifunza kula.
Umbo lake lipo kama kibuyu ,butternut ni chakula chepesi na laini kwa mtoto anaenza kufunzwa kula solid food ,lina lainisha tumbo na kumfanya mtoto kupata choo kwa urahisi kwa wale watoto wenye matatizo ya choo (constipation )linafaa zaidi.
Jinsi ya kupikwa
Butternut squash linanjia nyingi za kupikwa hapa nitakupa baadhi ya recipes unaweza mwandalia mtoto ,ukampumzisha kula viazi kila siku
Chemsha kwa dakika 10-15 likiiva mwaga maji weka maziwa ya baby formula (kopo) au maziwa ya mama nusu kikombe baada ya kukamua (pump) saga pamoja tayari kuliwa.
Butternut squash changanya na carroti 1 chemsha pamoja ikiiva saga na tayari kuliwa
Viazi vitamu changanya na butternut squash chemsha pamoja na kusaga
Zucchini chemsha pamoja na butternut ikiiva saga tayari kuliwa
HILI NDIO ZUCCHINI LINAUMBO LA TANGO
Butternut,kiazi ulaya,karoti na njegere kidogo pika pamoja weka butter au olive oil kidogo ikiiva saga tayari kuliwa.
Utakapo pika chakula cha mtoto tumia butter au olive oil kwa watoto walio chini ya mwaka 1
No comments:
Post a Comment