Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki moon ametaka wale waliohusika kwenye shambulizi la kumchoma mtoto Mpalestina katika eneo linalokaliwa na Israel la ukingo wa magharibi kufikishwa mbele ya sheria.
Msemaji wa Ban alisema kuwa kushindwa kushughulikia suala la ukwepaji wa sheria dhidi ya ghasia zinazoendeshwa na walowezi wa kiyahudi ndicho kimesababisha kutokea kwa shambulizi kama hilo.
Amesema kuwa kutokuwepo kwa mipango ya amani, sera za ujenzi wa makao na ubomoaji wa nyumba za wapalestina ni kati ya mambo ambayo yamesababisha kuwepo ghasia kati ya pande zote.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameahidi kuwa wale waliotekeleza kitendo hicho alichokitaja kuwa cha kigaidi watachukuliwa hatua za kisheria.
Ameelezea mshangao wake kutokana ni kile alichokitaja kuwa mauaji ya kikatili ambapo pia aliwatembelea wazazi wa mtoto huyo na nduguye ambao kwa sasa wanauguza majeraha mabaya hospitalini.
No comments:
Post a Comment