Dar. Chama cha ACT-Wazalendo wazindua rasmi kampeni zao kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.
Katika uzinduzi huo, mgombea wa Urais wa chama hich, Anna Mghwira ameahidi kuunda serikali ya umoja wa kitaifa endapo atashinda urais.
Alisema vyama vyote vya siasa na makundi mbalimbali ya kijamii yatajumuishwa kwenye serikali hiyo.
Pia mgombea huyo alitumia fursa hiyo kuainisha vipaumbele vya chama chake kuwa ni Hifadhi ya Jamii, Uchumi Shirikishi wenye kuzalisha ajira nyingi na bora. Vipaumbele vingine ni Afya na Elimu.
Kwa upande wake mshauri wa chama hicho, Prof Kitila Mkumbo aliwaeleza wananchi kwenye uzinduzi huo kazi za rais wa nchi kuwa siyo umeneja wa kusimamia miradi bali ni kutoa dira, misingi ya nchi na mwenye uwezo wa kutoa sera.
Alizitaja kazi nyingine za rais kuwa lazima awe mlinzi mkuu wa tunu za taifa ambazo ni umoja, usawa katika taifa, uadilifu, na demokrasia. Aliongeza kuwa rais anapaswa kuwa mfano bora wa binadamu mwenye kuleta sura ya taifa, pia uadilifu wa taasisi, yaani ni lazima atokane na chama cha siasa chenye uadilifu.
Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe alisema kuwa haiwezekani mabadiliko kuletwa na watu wanaotuhumiwa ufisadi, hivyo akawataka wananchi kukiamini na kukipigia kura chama cha ACT-Wazalendo ambacho ndicho chama pekee chenye dhamira ya kuleta mabadiliko ya kweli kwa watanzania.
MWANANCHI.
MWANANCHI.
No comments:
Post a Comment