NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
CHAMA cha ACT Wazalendo kimepanga kuanza kampeni zake rasmi Jumapili katika viwanja vya Mbagala Zakhiem, Dar es Salaam kwa ajili ya kumnadi mgombea Urais wa chama hicho na wagombea Ubunge katika majimbo yote.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Katibu wa Mipango na Mikakati wa ACT Habibu Mchange, alisema uzinduzi huo utahutubiwa na Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, Katibu Mkuu Samson Mwigamba na mgombea Urasi Anna Mghwira.
“Jumapili tutazindua kampeni kitaifa, tutamnadi mgombea urais, mgombea mwenza, wagombea ubunge kwa nchi nzima Tanzania Bara na Zanzibar, ratiba itaanza saa nne asubuhi,” alisema Mchange.
Wakati huo huo, chama hicho kimedai kufanyiwa rafu na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika matawi kwa kuondoa bendera zao na kuwavamia wanachama kwenye mikutano na kuwafanyia vurugu.
No comments:
Post a Comment