Monday 13 July 2015

WATU WASIOJULIKANA WAMEVAMIA KITUO CHA POLISI WAPORA SILAHA NA KUFANYA MAUAJI YA KINYAMA POLISI KADHAA WAPOTEZA MAISHA



Baadhi ya picha kutoka eneo la tukio.
WATU wasiojulikana wamevamia Kituo cha Polisi Stakishari kilichopo Ukonga jijini Dar es Salaam, jana usiku na kuua askari na raia kisha kupora silaha.
Kwa mujibu wa taarifa za awali ambazo bado hazijathibitishwa na Jeshi la Polisi ni kwamba watu hao walifika kituoni hapo wakiwa katika pikipiki wakidai kwamba walikuwa wamembeba mtu aliyepata ajali wakihitaji msaada wa polisi kabla ya kuwabadilikia ghafla na kuanza kuwashambulia kwa risasi.
Inadaiwa kuwa askari wanne wamepoteza maisha katika tukio hilo, wananchi wawili na mmoja wa watu hao.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova aliyesema atakuwa na mkutano na wanahabari kati ya saa 5 au 6 leo kwa ajili ya kutoa taarifa rasmi juu ya tukio hilo 
Habari kamili zitakujia pindi tutakapozipata 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!