Monday, 20 July 2015
WATANO WAKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO LA UVAMIZI NA MAUAJI YA POLISI WA KITUO CHA POLISI STAKISHARI JIJINI DAR
Polisi Jijini Dar es Salaam wamesema wamewakamata watu watano waliohusika na tukio la ujambazi katika Kituo cha Stakishari, pia silaha kadhaa zimekamatwa.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, ameapa kwamba Jeshi hilo litawakamata wale waote waliohusika na tukio hilo, pia amesema kama wapo watu waliohusika na tukio hilo wajisalimishe.
Silaha zilizopatikana ni SMG 7, Sar, 7, Risasi 28 za SMG zote za Kituo cha Polisi Stakishari, Pia wamekamata sanduku lenye fedha za Kitanzania milioni 170
Kamanda Kova amesema kuwa huo ni mwanzo wa msako mkali dhidi ya mtandao huo hatari wa kijambazi unaofanya matukio yake kwenye taasisi za kifedha,vituo vya polisi na hata kupora kwa kutumia pikipiki.Majambazi hao wanaishi porini na mjini kidogo huku wakitegemea mapato ya uhalifu wao kujikimu,amesema Kamanda Kova.
Kamanda Kva amesema kuwa kuanzia sasa uinzi utaimarishwa katika vituo vya polisi kutokana na hali iliyopo. Wananchi wakija usiku,watapaswa kurudi asubuhi. Pia,wananchi watakaokwenda vituoni wakiambiwa wasimame ili wahojiwe au wakaguliwe wafanye hivyo.
Kamanda Kova amesema kuwa majambazi watatu waliouwawa katika kurushiana risasi na polisi.Hakuna polisi aliyeumia wala kuuwawa. Kamanda Kova ameyataja hadharani majina ya majambazi wanaosakwa pamoja na kutoa picha zao zikiwa na majina pamoja na mahali wanapotembelea au kuishi.
Kimsingi, silaha na fedha zilizopatikana zimeonyeshwa. Pia,pikipiki zilizokamatwa zimeonyeshwa hadharani. Hongereni JESHI LA POLISI LA TANZANIA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment