Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa jimbo la Monduli akiingia kwenye ukumbi wa mikutano ndani ya hotel ya Bahari Beach jijini Dar,kwenye mkutano wa Wanahabari jioni ya leo.
Mh.Lowassa akiingia kwenye Hoteli Bahari Beach kwa ajili ya kutangaza adhima yake ya kujiunga na UKAWA. Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa ametangaza kujiunga rasmi na Umoja wa Katiba (UKAWA) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) .
Mh.Lowassa akiwa na viongozi wa UKAWA katika Hoteli ya Bahari Beach Hoteli jijini Dar es Salaam jioni ya leo mara baada ya kutangaza rasmi azma yake ya kujiunga na ukawa.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa katika Hoteli ya Bahari Beach Jijini Dar es Salaam jioni hii alipokuwa akitangaza azma yake ya kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA.
Mh.Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akiteta jambo na Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
1 comment:
aziz bilal22:47
1
Nawala wao sio mungu pia.Maji ukiisha yavulia nguo ni lazima uyaoge,koga maji mwanangu Lowassa tayari umeisha yavulia nguo .
Post a Comment