Zoezi la bomoabomoa katika maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam kupisha ujenzi wa bomba kubwa la maji limeendelea kuwakumba wakazi wa maeneo hayo ambao wamelalamikia mamlaka husika kufanya zoezi hilokwa kile walichodai kuwa ni ukomoaji jambo linalowasababishia hasara kubwa ya maghorofa yao kubomolewa.
ITV imeshuhudia zoezi hilo la ubomoaji wa jengo lenye ghorofa moja katika eneo la Tangi Mbovu likiwa linabomolewa kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kusafisha njia ya kupitisha mradi wa bomba kubwa la maji kutoka ruvu juu huku mmiliki wa jengo hilo Bwana Gilbart Lauwo akilalamikia zoezi hilo.
ITV imezungumza na afisa mahusiano na ufundi aliyekuwepo katika eneo hilo kusimamia utekelezwaji wa zoezi hilo Bwana Abel Chibelenje ambaye amedai kuwa zoezi hilo linafanyika kwa kufuata taratibu zote huku akielezea madhara yanayoweza kuwapata wakazi wanaojenga karibu nabomba hilo endapo kutatokea hitilafu baada ya mradi huo kupita ikiwa ni pamoja na maafa.
Mradi huo wa ujenzi wa bomba kubwa la kupitishia maji umekuwa ukisuasua kutokana na baadhi ya watu waliojenga katika njia ya kupitishia bomba hilo kukimbilia mahakamni jambo lililosababisha kwa kiasi kikubwa kuchelewa kukamilika kwa mradi huo kwa wakati ili kumaliza adha ya upatikanaji wa maji jijini Dar es Salaam kwa mujibu wa serikali.
CHANZO:ITV
CHANZO:ITV
No comments:
Post a Comment