Mapema wiki hii zilisikika taarifa ya lori la mafuta kuua zaidi ya watu 90 huko Nigeria ikiwa ni baada ya kuwa kwenye mwendo mkali na kugonga watu na magari yaliyokuwa kwenye kituo cha abiria.
Lakini leo Ghana nayo imeingia kwenye vichwa vya habari baada ya kituo cha mafuta kulipuka na kuua watu wanaokadiriwa kuzidi 90 katika mji mkuu wa nchi hiyo Accra.
Mlipuko huo umetokea baada ya mvua kubwa iliyosababisha mafuriko katika maeneo mengi ya mji huo ambapo pia imewaacha watu wengi bila makazi huku sehemu kubwa ya mji ikiwa gizani kutokana na kukatika kwa umeme.
Idadi ya watu waliofariki huenda ikaongezeka kwani watu wengi wamepoteza maisha baada ya kuwepo kituoni hapo wakijikinga na mafuriko yaliyotokea na huenda idadi ikaongezeka kutokana na baadhi ya miili kuwa bado haijapatikana.
No comments:
Post a Comment