Wednesday, 3 June 2015

WATU ZAIDI YA 400 WAZAMA NA MELI CHINA

Vikosi vya uokoaji tayari vimeelekea kwenye eneo la tukio
Meli iliokuwa imewabeba zaidi ya watu 450 imezama baada ya kukumbwa na upepo mkali katika mto Yangtze kusini mwa China.


Kwa mujibu wa shirika la habari la serikali Xinhua watu wanane wameokolewa mpaka sasa na kazi inaendelea ya kuwaokoa abiria wengine.
Waziri Mkuu Li Keqiang anaelekea katika eneo la tukio.
Meli hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka mashariki mwa mji wa Nanjing kwenda Chongqing kusini magharibi ilipozama.
Meli hiyo, Dongfangzhixing - au Nyota ya Mashariki - ilikuwa imewabeba abiria wa Kichina 405, wafanyakazi watano wa shirika la usafiri na wafanyakazi 47 wa meli hiyo.
Nahodha na mhandisi mkuu, ambao ni miongoni mwa waliokolewa wamenukuliwa wakisema kuwa meli hiyo ilikumbwa na kimbunga na kuzama haraka.
Kazi ya uokoaji imekwamishwa na upepo mkali na mvua kubwa. Meli hiyo ilizama katika kaunti ya Jianli katika jimbo la Hubei.
Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la serikali ya China, meli hiyo inamilikiwa na Shirika la Meli la Chongqing Eastern ambalo linaendesha shughuli za utalii katika maeneo matatu ya vivutio katika mto Yangtze.
Waliokuwa katika meli hiyo wengi wao walikuwa watalii wenye umri kati ya miaka 50 na 80 wakiwa katika safari ya kitalii iliyokuwa imeandaliwa na kampuni ya Shanghai.
Habari zinasema meli hiyo imepinduka.
Watu ishirini na wawili waliufa katika mto huo mwezi Januari, wakati boti iliyokuwa katika majaribio kuzama karibu na Zhangjiagang, katika jimbo la Jiangsu.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!