Tuesday, 2 June 2015

WANAHARAKATI WA BURUNDI WAWATAKA MARAIS WA EAC KUTUMIA NGUVU ZA KIJESHI KUMNG’OA NKURUNZIZA

Mwenyekiti wa Taasisi ya Burundi Women and Girls Movement, Prof Christine Mbonyingingo (kati) akizungumza na wanahabari.

 Wanaharakati hao wakiwa katika mkutano na wanahabari (hawapo pichani).
 Rais wa Taasisi ya Coalition of Civil Society for Election Monitoring, Justine Nkurunziza akifafanua jambo.
  Mwanasheria kutoka nchini Burundi, Janvier Bigirimana akijibu maswali ya wanahabari. Kushoto ni Prof. Christine Mbonyingingo


Wanaharakati pamoja na taasisi mbalimbali za kutetea haki za binadamu kutoka nchini Burundi zimewataka marais wa umoja wa nchi za afrika mashariki (EAC) kutumia nguvu za kijeshi kumng’oa rais anayegombea muhula wa tatu nchini humo kinyume na katiba ya nchi hiyo, Pierre Nkurunziza.
Wakizungumza na waandishi wa habari leo hii katika ukumbi wa Hoteli ya New Africa jijini Dar, wanaharakati hao kutoka Taasisi ya Civil Society na Burundi Women and Girls Movement, walisema kuwa wameamua kufikia hatua ya kuomba msaada wa kijeshi kutokana na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanya na jeshi la nchini humo.

Wanaharakati hao ambao wameweka kambi yao nchini Tanzania walidai kuwa kutumika kwa nguvu ya kijeshi kutoka nchi jirani shirikisho la Nchi za Afrika Mashariki ndiyo suluhisho pekee la kurejesha amani nchini humo huku akiwataka marais wa nchi hizo jirani na Burundi kutoyafumbia macho mateso ya raia wa Burundi.

Mbali na hayo wanaharakati hao walidai kusikitishwa na kitendo cha wanaharakati wenzao wa Burundi kuzuiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar na kutakiwa kuondoka mara moja nchini japo kuwa walikuwa na nyaraka zote za kusafiria.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!