Sehemu iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya kutangaza nia ya kugombea urais katika Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Frederick Sumaye akitangaza nia ya kugombea urais mbele ya wananchi waliohudhuria mkutano huo leo.
Meza kuu, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Ester Sumaye (kushoto) Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye (katika) Mwenyekiti wa UVCCM wa Kinondoni, Shabani Uronu, pamoja na Katibu Mwenezi CCM, Kata ya Kiluvya, Juma Semindu.
WAZIRI Mkuu Mstaafu Mhe. Frederick Tluway Sumaye leo ametangaza nia ya kugombea urais wa Tanzania kwa mwaka wa 2015 kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza leo mbele ya wananchi na wanahabari katika Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency (zamani Kilimanjaro Hoteli) jijini Dar es Salaam, Sumaye amesema kuwa ameamua kutangaza nia ya kuwa mgombea urais kutokana na alivyoweza kujipima mwenyewe, kujishauri na kutafuta ushauri kutoka kwa watu wengine na kuona kweli anafaa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alisema kuwa amejitathimini na kuona kuwa yeye ndiye anayetosheleza kuwa kiongozi wa nchi hii kutokana na jinsi alivyoweza kuongoza nchi hii akiwa Waziri Mkuu kwa zaidi ya miaka 9 na hivyo anastahili kuiongoza nchi.
Aliongeza kuwa amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi katika utumishi wa umma, kama ubunge, unaibu waziri, Uwaziri na hatimaye kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.
“Katika uongozi wangua nilijitahidi sana kusimamia uchumi wa taifa kama vile, kusimamia uchumi, kuvunja Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam iliyokuwa ikiongoza kwa uchafu wa mazingira miaka ya 1996, kutengeneza madawati kwa shule zote za msingi, kuweka televisheni ya taifa, mpango wa maendeleo Elimu (MMEM) na mambo mengine, ”alisema.
Vilevile alieleza juu ya kufanya kazi kwa muda huo wote katika ngazi mbalimbali kuwa ni dhahiri nchi anaifahamu pamoja na shida za wananchi pamoja na matatizo yao anayajua, kila eneo na kila kanda hivyo akiteuliwa kuwa rais hatahitaji kujifunza juu ya nchi ya Tanzania.
Wakati akizidi kufafanua alieleza malengo yake endapo akiteuliwa kuwa rais kuwa lazima atazingatia mambo yafuatayo ili kuweka uchumi imara katika nchi yetu ya Tanzania ikiwa ni pamoja na kulinda muungano pamoja na amani na utulivu, kuimarisha uchumi, kupambana na maovu ya rushwa kama vile ufisadi na madawa ya kulevya na mauaji, kuboresha huduma za jamii na ajira pamoja na michezo.
Waziri Mkuu Mstaafu alipoulizwa swali juu ya ambao wote tayari wamekwisha tangaza nia ya kugombea urais kwa mwaka 2015 kuwa nani anamwona kuwa kinara zaidi yake alisema kuwa yeye ndiye anafaa kuwa kiongozi wa nchii hii kwani wote waliokwisha tangaza haoni kama wana imani na kuongoza nchi yetu.
1 comment:
aziz bilal8:50 PM
1
Reply
Hata mimi pia naitaka hiyo nafasi ninaweza nikawa rais nitagombea namimi nimo ktk kinyang'anyiro hicho ka mambo yenyewe ndiyo hayo hata mimi nitatangaza hivi karibuni.
Post a Comment