Mkulima darasa la saba Eldoforce Bilohe amekua kituko baada ya kukaribishwa CCM makao makuu DODOMA na kisha kushindwa kukamilisha zoezi kwa kukosa fedha.
Amepata ushabiki mkubwa kutoka kwa wananchi na waandishi. Kaingia kwa miguu na kaondoka kwa miguu kuelekea benki hata hivyo amechelewa kurudi.
Hata hivyo, Bilole (43) aliyetembea kwa miguu huku akiwa amebeba chupa mbili za maji, mfuko wa plastiki na begi dogo jeusi, hakuweza kuchukua fomu kutokana na kufika katika ofisi hizo akiwa hana Sh1 milioni za malipo.
Baadaye alifanikiwa kulipa ada hiyo na sasa amepangiwa kuchukua fomu yake leo saa 10.00 jioni.
“Nilikuwa Benki ya CRDB, nikaitwa ofisi za chama nikaona nije ili nisikilize wito, kabla ya kuchukua fedha kwanza,” alisema Bilole aliyefika peke yake kwenye ofisi hizo.
Bilole alisema anajua Mungu atamwezesha kukabiliana na watu wengine walioomba ridhaa ya chama kuwania nafasi hiyo.
Alipoulizwa sababu ya kufika pekee yake katika ofisi hizo, alisema hajawahi kuwa na makundi ambayo yameonekana kwa makada wengine... “Nadhani naweza ndiyo maana nimejitokeza kuwania nafasi hii. Nitawavusha kuwapeleka kwenye nchi ya ahadi,” alisema na kuongeza kuwa alijiunga na chama hicho mwaka 2003 huku akiahidi kuhakikisha anainua uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo.
Bilole ni nani?
Bilole alizaliwa Januari 21, 1971 katika Kijiji cha Mtala wilayani Kasulu mkoani Kigoma na anajishughulisha na kilimo.
No comments:
Post a Comment