Waziri wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli akionesha fomu ya kugombea urais 2015
Waziri wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli akionesha fomu ya kugombea urais.
Waziri wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli akisaini mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea urais.
Waziri wa Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli leo amechukua fomu ya kugombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi na kuacha gumzo kwa waandishi pamoja na wananchi waliohudhuria kumsikiliza katika ukumbi wa mikutano wa NEC mkoani Dodoma leo.
Magufuli amezua gumzo kufuatia kugoma kuongea na waandishi wa habari pamoja na wananchi waliohudhuria katika tukio la kuchukua fomu ya kugombea urais.
Akizungumza mara baada ya kupokea fomu ya kugombea Urais, Magufuli amesema kwamba hajui kwenye fomu hizo kimeandikwa nini hivyo kuomba muda zaidi wa kuzisoma na kuahidi kuwa atazungumza na waandishi wa habari muda ukifika.
Katika hatua nyingine Magufuli amesema kwamba moja ya kipaumbele chake ni kutekeleza ilani ya chama Cha Mapinduzi katika kitabu cha ilani alichokishika wakati akichukua fomu ya kugombea urais.
No comments:
Post a Comment