Monday, 15 June 2015

KECHI OKWUCHI MWANADADA ALIYETIBIWA KWA KUFANYIWA OPASUAJI MARA 75

HUJAFA hujaumbika, ndivyo ninavyoweza kumzungumzia Kechi Okwuchi, ambaye amefanyiwa upasuaji mara 75 ili kunusuru maisha yake baada ya kunusurika katika ajali ya ndege.

Lakini namna nyingine ya kumuelezea dada huyo ni ujasiri, kwani ameonesha wazi kuwa ulemavu si sababu ya kushindwa katika jambo lolote lililopo ka- tika ndoto ya maisha ya mwanadamu yeyote.
Kechi aliyenusurika katika ajali mbaya ya ndege ya Shirika la Sosoliso, inakwenda Port Harcourt ikitokea mjini Abuja, nchini Nigeria Desemba 2005, miaka kumi baadaye amehitimu Shahada ya Kwanza akiwa amepata daraja la kwanza na kuongoza wenzake wa mataifa mbalimbali waliosoma pamoja.
Kechi amehitimu katika Chuo Kikuu cha St Thomas Houston Texas Mei 16, mwaka huu na kutunukiwa Tuzo ya Sita ya Heshima ya Jamii katika masomo yake na kuwa mmoja kati ya wanafunzi waliofanya vizuri sana katika mchepuo wa Uchumi.
Pia alichaguliwa kuhutubia darasa la wanachuo hao. Desemba 10, mwaka 2005 ndege ya Shirika la Ndege la Sosoliso ikitokea Abuja, ilianguka kusababisha vifo vya watu wakiwemo wanafunzi 60 wa Shule ya Loyola Jesuit.
Miaka 10 baadaye mwanamke huyu kijana anaelezea hadithi yake ya kusisimua ya namna alivyopata nguvu na ujasiri wa kuendelea na maisha. Kechi Okwuchi anasema yeye ni mtoto wa kwanza katika familia ya watu wanne ambao ni baba, mama na mdogo wake wa kike.
Alijiunga na Chuo cha Loyola Jesuit, Abuja kwa ajili ya elimu ya sekondari. Baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha St Thomas, Houston, Texas, Marekani kwa ajili ya elimu ya juu.
★Utoto
Mwanadada huyu anasema maisha yake ya utoto yalikuwa ya kuvutia na anawashukuru wazazi wake na wakati wa likizo, alikuwa akitumia muda huo na binamu zake na familia mjini Lagos.
Kechi anasema kwa maelezo ya mama na baba yake, alikuwa mtoto aliyeridhika na mwenye furaha. “Nakumbuka nilikuwa mzungumzaji sana (mpaka sasa) na walimu wangu walikuwa wakiandika kwenye ripoti zangu kuwa ndio, ana akili, lakini anazungumza sana!” Anaongeza.
Kwa mujibu wa Kechi, alikuwa mtoto pekee wa familia kwa miaka 11, lakini hakuwahi kujisikia mpweke kwa kuwa alikuwa na marafiki wazuri na binamu wengi.
Anasema baada ya kuzaliwa kwa mdogo wake wa kike mwaka 2000, maisha yalibadilika kwa kuwa; “nilitoka kuwa ‘binti pekee’ na kuwa ‘dada mkubwa’ na nilijisikia ajabu na furaja kumlea mdogo wangu.”
★Ajali ya Ndege
Kechi anakumbuka alipokuwa katika ndege aliyopata nayo ajali, dakika 15 kabla ya kumalizika kwa safari, rubani alitangaza kwamba walikuwa karibuni kutua kwenye uwanja wa ndege wa Port Harcourt.
“Nakumbuka nilikuwa nimekaa siti ya katikati na rafiki yangu wa karibu Toke alikuwa na kaka yake upande wangu wa kulia. Hali ya ndege ilibadilika ingawa sikuwa na hofu mpaka abiria mmoja alipopiga kelele akihoji, “hivi hii ndege inajaribu kutua?’” “Sikuweza kuona nje kutokana na eneo ilipokuwepo siti yangu, lakini sasa nadhani ilikuwa afadhali hivyo.
Wakati huo kilichokuwa kikitokea ni hali ya ajabu ajabu. Nilimgeukia Toke na tukashikana mikono, nilimwambia ‘labda tuombe.” “Ghafla nilisikia sauti ya kukwaruza masikioni kwangu na ninachojua kitu kilichofuata, ilikuwa kuamka nikiwa katika Hospitali ya Milpark, Afrika Kusini.
Mpaka sasa sikumbuki hali halisi ya ajali ilivyokuwa.” akirudiarudia kuita jina lake, akimuuliza kama anamsikia. “Wakati nikijaribu kuamka, nilijisikia ganzi na kuchoka sana kwa namna ambayo nilishindwa kuelewa.
Hatimaye niliona umbo la mama yangu; nilimuona akitabasamu, nilitamani nione uso wa mama yangu vizuri, kwa sababu nilikuwa naona ukungu ukungu.
“Wakati nimelala pale, nilijua mambo ni mabaya sana, lakini alikuwa pembeni yangu na alinifanya nijisikie ahueni, nashindwa hata kuelezea,” anasema Kechi.
Anasema marafiki na familia yake, upendo wao, uwepo wao, kimwili na kihisia, maombi yao na wale wote waliojitolea kumuombea, ndio wanaomfanya aendelee kustahimili.
Kechi anasema alifahamu kipindi cha kupona kila baada ya upasuaji si rahisi, lakini pia alifahamu kwa uzoefu wake si tu Mungu alimvusha katika operesheni hizo, lakini pia alimuwezesha katika kipindi cha uponyaji.
★Kuingia chuoni
Anasema kuomba nafasi ya chuo ilikuwa jambo la kujifurahisha kwake. “Nilikuwa nje ya chuo muda mrefu hadi kufikia 2010, nilikuwa na shauku ya kurudi shule kwa sababu siku zote shule ilikuwa jambo muhimu kwangu, kwa hiyo hisia hii ilikuwa ya kwanza kwangu.”
Kechi anasema aliomba nafasi ya shule katika vyuo vitatu vya Texas, Marekani kikiwemo chuo ambacho amehitimu sasa na kuongeza kuwa alitakiwa kuhamia Chuo Kikuu cha Rice baada ya muhula wa kwanza, lakini alivutiwa na kampasi ya UST kwa hiyo alibakia hapo kwa kile alichoeleza kampasi hiyo inamkubusha Chuo cha Loyola “Naweza kusema maisha ya chuoni yalikuwa na changamoto na ya kuchekesha.
Tofauti na uzoefu wangu nilipokuwa sekondari kwa sababu nilijifunza vitu ambavyo ndio navutiwa navyo. Kama mwanafunzi sina cha kuomba zaidi,” anasema.
★Hali ya kushangaza
Kechi anasema kutoka na hali yake, watu wamekuwa wakimuangalia kwa mshangao na ilibidi akubaliane na hali hiyo. “Ninapofikiria, kama hali ingekuwa kinyume na mtu aliyeungua angekuwa akipita mbele yangu mtaani, ningemtazama mara moja; ni hali ya kawaida kibinadamu.
Kwa hiyo sijali watu wakinishangaa. “Mara nyingi watu huniuliza moja kwa moja kilichonitokea na mimi huwa sijibu … nadhani naweza kusema mtazamo chanya unafanya kuwa rahisi kwa wengine kukuchukulia kawaida, jambo ambalo nalishukuru sana,” anasema mwanadada huyu jasiri.
Kechi anasema hakuna kitu kizuri kama maombi kwani kinaongeza imani na ujasiri kwa kuwa kilimsaidia kumtuliza mambo yalipokuwa magumu.
Anasema kwa uzoefu wake jambo moja alilojifunza kupitia hali yake hiyo ni kuthamini imani, lakini pia familia na marafiki zake ambao wakati wote wamekuwa jiwe la yeye kuegemea.
“Bila vipengele hivyo vitatu, nisingefika mbali hivi, lakini nisingeweza pia kuwa mtu huyu sasa kiakili,” anasema. Anasema kwa uhakika limekuwa jambo gumu kwa familia yake na kwamba tabia ya kuwa na matumaini ameipata kutoka kwenye familia yake.
Makala haya yametafsiriwa kutoka vyanzo mbalimbali vya kimataifa.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!