Naamini msingi mkubwa wa maendeleo ya Watanzania walio wengi hasa maskini kama mimi ni kupata usimamizi mzuri wa halmashauri zetu.
Hii kusema kuwa, hapo ndipo miradi mbalimbali inayowagusa wananchi wa kawaida inapoibuliwa na kutekelezwa. Vivyo hivyo, kiasi kikubwa cha pesa za bajeti ambazo ndiyo kodi zetu wananchi zinapopelekwa kwa ajili ya kuleta mabadiliko chanya kwa jamii, hivyo kwa kutafakari hayo na hali halisi ilivyo katika halmashauli zetu, nimegundua kuwa mnaweza kuwa na mbunge mzuri, mpambanaji na anayehakikisha mnapata mafungu ya kutosha kwa ajili ya miradi muhimu kama vile elimu, maji, afya na mengineyo lakini kwenye halmashauri mkakosa wasimamizi bora hatimaye zikaishia kwenye kinywa cha watu wabinafsi wale wasioitakia mema Tanzania. Kwa maelezo hayo, ndipo nilipofikia uamuzi wa kuona kama kijana niliye na fikra chanya za kimabadiliko na tija ninajukumu la kuwa sehemu ya chachu ya maendeleo katika halmashauri ya Mkuranga mkoani Pwani kupitia Kata ya Tengelea.
Diwani kazi yake kubwa ni kuisimamia halmashauri na kuwa kichochezi cha mabadiliko katika Kata. Hivyo mimi nikiaminiwa na kwa kupewa ridhaa, nitasimama pamoja na wananchi wenzangu ili niwaongoze na ninaamini kuwa ndani ya miaka mitano tutatakiwa kuweka nguvu kwenye mambo yafuatayo:
1. Elimu yenye Tija na Ushindani
2. Huduma ya Afya
3. Maji Safi na salama
4. Miundombinu na Nishati
5. Masoko
6. Fursa za kijasilimali na kuwa mfumo wa kuinua vipato kwa wanajamii,
Naamini tutafanikiwa kuyafanikisha hayo katika kata kwa kupitia fursa zifuatazo:
a/ Kwa kuwa maendeleo ni yetu sote lazima tuhamasishane na kuelimishana sisi wananchi kubuni na kuibua miradi
b/ Kuhamasisha kuchangia kwa hiyari wananchi juu jambo tulilolibuni na kuliibua ili iwe chachu ya kuzishawishi mamlaka za juu kuongeza nguvu
c/ Kutengeneza mfumo na wanajamii kuhusu Tozo za mauzo ya mashamba na vitu kuingia katika uboreshaji wa miundombinu na majengo Kusimamia mafungu ya maendeleo yaliyotengwa na halimashauri kutoka wizara husika zinafika sehemu husika na kufanyiwa kazi kwa haraka
e/ Kushirikisha sekta binafsi na wadau mmoja mmoja kuhusu ustawishaji wa maendeleo.
Kwa maelezo na kupitia tafakuri hiyo nimeshawishika ifikapo Tarehe 15 July 2015 kwenda kuchukua fomu ya kuwaomba wanaCCM wenzangu wa Kata ya Tengelea wanipe ridhaa ya kwenda kwa wananchi kuanzia Agost 22 kuomba kupigiwa Kura ya NDİO ya kuwa Diwani wa kata ya Tengelea, Ninaamini kuongoza ni kupokea fikra za waliowengi na kuziwakilisha katika vyombo vya maamuzi, kisha kuwa msimamizi wa upatikanaji wa haki hizo au majibu ya hoja hizo kisha kutoa mrejesho kwa wananchi na kusimamia utekelezaji ulitukuka. Mwisho japo sio mwisho kwa umuhimu "Uongozi ni ubunifu unahitaji fikra yakinifu,"
Nawasilisha
Mwalimu Ismail k. Mussa
No comments:
Post a Comment