Baada ya kujifunza maumbo (forms) mawili kati matano ya vitenzi (verbs) vya Kiingereza ambayo tutayatumia katika kuunda’English tenses’, leo tutaendelea kujifunza maumbo zaidi. Kabla ya kuendelea tujikumbushe baadhi ya vitenzi na maumbo yake.
Clean (safisha) cleans cleaning cleaned
cleaned
Run (kimbia) runs running ran run
Tie (funga) ties tying tied tied
Leo tutajifunza kuhusu umbo la tatu . Umbo hili huundwa kwa kuongeza –ING kwenye mzizi wa kitenzi. Sasa tuone mifano na kanuni zake.
Kanuni 1: ongeza –ing kwenye mzizi wa vitenzi vilivyo vingi. Mfano:-
• carry carrying
• try trying
• open opening
• walk walking
Kanuni 2: vitenzi vingi vinavyoishia na –e inabidi uondoe –e kisha ongeza –ing. Mfano;-
• close closing
• ride riding
• write writing
Kanuni 3: kitenzi kikiishia na –ee unachokakiwa kufanya ni kuongeza –ing . mfano:-
• agree agreeing
• free freeing
Kanuni 3: vitenzi vinavyoishia na –ie badili –ie iwe –y kisha ongeza –ing. Mfano:-
• lie lying
• tie tying
Kanuni 4: vitenzi vinavyoishia na –ic ongeza –k kisha ongeza –ing. Mfano:-
• panic panicking
• traffic trafficking
Kuna baadhi ya vitenzi ambavyo kabla ya kuongeza –ing ni lazima herufi za mwisho za mzizi wa kitenzi ziwe mbili. Mfano wa vitenzi hivyo ni ;-
• swim swimming
• shut shutting
• get getting
• rot rotting
• rap rapping
• begin beginning
exercise 1
Ongeza –ing kwenye mzizi wa vitenzi vifuatavyo.
1. take off ----------
2. dry ----------
3. leave ----------
4. die ----------
5. see ----------
6. fly ----------
7. picnic ----------
8. stop ----------
9. sleep ----------
10. hit ----------
Exercise 2
Andika mizizi ya vitenzi ambayo maumbo yake yenye –ing ni kama ifuatvyo: mfano
studying, arriving, helping, shopping, advising, using.
CRD: MWALIMU SAID MLOWA
No comments:
Post a Comment