Thursday, 7 May 2015

WANASIASA NCHINI WAONYWA KUHUSU SHILINGI


WANASIASA wameaswa kuwaachia wataalamu wa uchumi ili waweze kushughulikia suala la kuporomoka kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania.

Aidha, imeelezwa kuwa wazalishaji wa Tanzania wanapaswa kuitumia vyema fursa ya kushuka kwa shilingi kuboresha bidhaa za ndani, kwani zitauzika zaidi badala ya bidhaa za nje.
Hayo yalisemwa jana jijini hapa, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk Charles Kimei alipokuwa akizungumzia Mkutano Mkuu wa 20 wa wanahisa wa Benki ya CRDB, unaotarajia kufanyika hapa na kushirikisha zaidi ya wanahisa 30,000.
Alisema suala la kuporomoka kwa shilingi ya Tanzania ni wakati mwafaka sasa kwa Watanzania sambamba na wawekezaji kununua bidhaa za nchini ili Shilingi iweze kukua badala ya kununua bidhaa za nje zinazosababisha dola kupanda.
Alisema kushuka kwa shilingi ni neema kwa wazalishaji wa ndani kwani wakiimarisha bidhaa zao zitanunuliwa na kuonya kuwa, suala la uchumi lisiingizwe katika masuala ya siasa.
“Naomba tuache wataalam wa uchumi pamoja na serikali katika kulishughulikia suala hili,” alisema.
Pia alisema benki hiyo ipo vizuri katika huduma za Tehama pia inajivunia mafanikio makubwa ya kiutendaji na ya kifedha kwa mwaka 2013 licha ya changamoto mbalimbali lakini pia imepiga hatua katika maeneo yatakayoleta matokeo mazuri mbeleni.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!