Monday, 18 May 2015

TISA WAUAWA KATIKA SHAMBULIO MAREKANI

Eneo ambapo shambulio hilo limefanyika.


Migahawa ukiwa umefungwa baada ya tukio hilo kutokea.
Polisi akiangalia hali ya usalama katika eneo hilo.
Baadhi ya watu waliokamatwa kwa kuhusishwa na shambulio hilo.
Polisi nchini Marekani wamesema kuwa watu tisa wameuawa katika shambulio lililotekelezwa na watu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki katika mgahawa wa Twin Park uliopo katika jimbo la Texa mjini Waco.
Hata hivyo watu wengine 18 walijeruhiwa vibaya na kupelekwa hospitali kupatiwa matibabu kutokana shambulio hilo.
Maofisa wa serikali katika mji huo wanasema kuwa, walibaini mkusanyiko kati ya watu watano walioonekana kupanga jambo lisilo la kawaida.
Watu waliokuwa katika mgahawa huo walijificha katika chumba cha majokofu katika harakati za kujiokoa kabla ya kusaidiwa na Polisi kutoka katika eneo hilo.
PICHA NA DAILY MAIL NEWS

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!