Sunday 31 May 2015

PANGANI KINARA WA UGONJWA WA MABUSHA



Wilaya ya Pangani Mkoa wa Tanga imetajwa kuwa ni kinara kwa kuwa na wagonjwa wengi wanaougua mabusha kati ya wagonjwa 400 waliogundulika 50,000 ni wazee kuanzia umri wa miaka 45 hadi 80.



Hayo yalisemwa Jijini Dar es Salaam na Mratibu wa Kampeni za kitaifa za Kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dk.Upendo Mwingira alipokuwa akizungumza kwenye mafunzo yaliyoandaliwa kwa ajili ya wanahabari ugawaji wa dawa za mabusha na matende katika Jiji la Dar es Salaam na Mwanza zoezi litakaloanza juni 22 mwaka huu hadi 26.

Aidha, Dk.Mwingira aliwataka wakazi wa majiji hayo kuchangamkia kunywa dawa hizo ambazo zitatolewa bure kwa kuwa imeelezwa kuwa watanzania wote wapo hatarini kuambukizwa ugonjwa huo wa mabusha na matende.


Alisema walipofanya operesheni ya upasuaji mkoani Tanga wagonjwa wengi walijaa ikiwa idadi kubwa inatokea wilaya ya Pangani huku wengi wao wakidai kuwa watu wa Pwani wanasema kuwa na mabusha ni heshima dhana ambayo alisema ni mila potofu.

Aliongeza kuwa ugawaji wa dawa kwa mtu mmoja mmoja utasababisha kukinga na kutibu jamii husika walio katika mazingira hatarishi na kutoa wito kwa wakazi hao kujitokeza kwa wingi kumeza dawa .

Alisema ugonjwa huo husababishwa na minyoo wadogo wadogo ambao huishi kwenye mfumo wa maji ya damu ya binadamu na huenezwa na mbu wote aliyataja baadhi ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ni mabusha,matende,kichocho,minyoo tumbo na Trakoma.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!