Dkt. Christine Mbunyingingo Mwenyekiti wa wanawake na wasichana katika harakati za usawa Nchini Burundi, Akiongea na waandishi wa Habari jana usiku .
*****
Mwenyekiti
wa vuguvugu za Maandamano Burundi kwa Mara ya kwanza amefika Nchini
Tanzania ili kuweza kushuhudia Mkutano wa Dharula kati ya viongozi
watano wa Jumuia ya Afrika Mashariki kuhusu nchi ya Burundi ambayo sasa
imeingia katika machafuko baada ya Rais aliyepo Madarakani kutaka
kuongeza muda wake.
Akiongea
na Waandishi wa Habari usiku huu Mkuu huyo wa vuguvugu wa Burundi
amesema kuwa wananchi hawaridhiki na Rais wao kuendelea kuwa madarakani
ambapo hata sheria na katiba hairuhusu na pia sasa ni wiki ya tatu
ambapo wananchi wanaendelea kupinga Rais kuendelea kuwania kwa Muhura wa
Tatu.
Amezungumzia
juu ya waandamanaji baada ya wiki tatu bado wapo barabarani ambapo
wameweza kuwa ni kiungo, wameweza kuwa ni njia kwa sababu wanadai
kumekuwa na mabadiriko kuhusu Rais wao, na kuwashukuru waandamanaji hao
kwa kuonesha moyo wa uzalendo na kuwa wameweza kudhihilisha na kuwa
walikuwa ni watulivu na kutulia kungoja utekelezaji wa mambo ambayo
yamezungumziwa.
Amesema
kwamba anaomba vurugu hizi zipate kwisha ambapo watu zaidi ya laki
mbili wamekimbia nchi na anaomba vurugu ziishe ili wapate kurejea nchini
kwao.
Pia
ameiomba Jumuia ya kimatafa iweze kufuatilia kwa karibu hali
inayoendelea kwa sasa Nchini Burundi ambapo jumuia iyo tangia zamani
imeweza kusimamia mambo ya usalama nchini Burundi na amani ili Burundi
iweze kufikia malengo ya Mkataba wa amani wa Arusha na kufikia malengo
ya katiba ambayo ndio uti wa mgongo wa taifa hilo.
Kuhusu jaribio la Mapinduzi kiongozi huyo amesema hayupo Miongoni mwa wale ambao wameandaa tukio hilo
Kuhusu
jambo baya alilofanya Rais wa Burundi Kiongozi huyo amaesema kwamba ni
kuongezea Muhula wakati tayari alisha tawala kwa Miaka 10, na katika
miaka hiyo alishindwa kuweka usawa baina ya warundi, hajatekereza swala
la haki za Binadamu , aliongeza kuwa Muhura wake ni Muhura baki na
Haramu hauko sambamba na Katiba wala Sheria ya Burundi pamoja na Mkataba
wa Arusha na angetekeleza yote hayo hizi vurugu zisinge kuwepo. Pia
hata makubaliano ya Arusha yanasema hakuna Rais ataenda Mihula mitatu.
Pia warundi wanafanya hivyo kwa sababu hawataki shuhudia tena Damu
inamwagika.
Mwisho amewaomba Marais watano wamalize salama Mkutano na kuhakikisha maamuzi yote yanafanyiwa kazi.
Nae
Mwenyekiti wa wanawake na wasichana katika harakati za usawa
amewashukuru kwa uvumilivu wao na kuendelea kupinga Rais wao kuendelea
kuwa madarakani kwa awamu ya Tatu.
No comments:
Post a Comment