KWA mara nyingine mgomo wa mabasi yaendayo mikoani na mabasi madogo (daladala) jijini Dar umeibuka na kuwafanya wananchi watumiao usafiri huo kubaki katika hali ya sintofahamu kwa kushindwa kufanya shughuli zao za kila siku.
Mgomo huo umechukua sura mpya baada ya madereva kudai kuwa serikali imekiuka ahadi waliyopewa na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka kuwa hawatasoma kila baada ya miaka mitatu pindi wanapotaka kuhuisha leseni zao.
Mbali na madai hayo, madereva hao wameweka mgomo kwa kigezo cha kushinikiza waajiri wao wawape mikataba ya kudumu. Mwandishi wetu amezunguka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar na kujionea hali halisi ya mgomo wa mabasi ya mikoani pamoja na daladala zikiwa hazifanyi kazi.
Mwanahabari wetu aliyeambatana na Timu wanahabari wa Global TV Online, alifika eneo la Stendi ya Kimara-Mwisho na kukuta wananchi wakitumia usafiri bodaboda na Bajaj kwenda katika sehemu zao za kazi huku baadhi yao wakieleza usumbufu mkubwa walioupata kutokana na mgomo huo.
“Kimsingi sisi wananchi mgomo huu unatuumiza zaidi. Mimi nafikiri wahusika wa pande zote mbili wanapaswa kuchukua hatua za haraka ili kutunusuru sisi tunaotumia usafiri huu lakini pia uzalishaji wa taifa,” alisema Juma, mkazi wa Kimara-Mwisho.
No comments:
Post a Comment