Sunday, 10 May 2015

BAJETI YA SERIKALI KUSOMWA JUNI 11

BAJETI Kuu ya Serikali itasomwa Juni 11, mwaka huu katika kikao cha 10 cha Mkutano wa 20 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, unaotarajia kuanza Jumanne ijayo mjini Dodoma.


Bunge hilo linalotarajiwa kumalizika Juni 27, litatanguliwa na kuwasilishwa kwa bajeti za wizara zote 24 kwa kuanzia na ile ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais, ambazo zitajadiliwa na kupitishwa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Bunge jana, Ofisa Habari wa Bunge, Prosper Minja, alisema bajeti hiyo kuu itasomwa siku hiyo saa 10 jioni ambapo asubuhi kutatolewa taarifa ya mipango ya Serikali.
“Bajeti ya Serikali itajadiliwa kwa siku saba, huku wizara nyingine zikipangiwa muda maalum wa kujadiliwa na kupitishwa,” alisema.
Minja alisema katika kikao hicho ambacho ni maalumu kwa ajili ya bajeti kitakuwa na vipindi vya maswali na majibu ambapo maswali 295 yataulizwa na kupatiwa majibu.
Minja alisema kutajadiliwa na kupitishwa kwa Muswada wa Sheria ya Fedha za Matumizi wa mwaka 2015 na Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2015

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!