Watoto wanaodaiwa kubakwa na baba yao. Akizungumza na gazeti hili kwa tabu hospitalini hapo, mtoto mwenye miaka 14 anayesoma darasa la nne, Shule ya Msingi Mkombozi (jina limehifadhiwa) alisema alianza kubakwa siku nyingi na baba yake huyo huku siku zingine akifanyiwa ukatili huo kwa usiku kucha huku akipata maumivu makali.
Watoto wa kike wawili wenye umri wa miaka 8 na 14, wakazi wa Unga Limited jijini hapa, wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa Mount Meru baada ya kuharibiwa vibaya sehemu zao za siri kwa madai ya kulawitiwa na kubakwa na baba yao mzazi waliyemtaja kwa jina moja la Ezekiel, Uwazi linakupa zaidi.
MSIKIE MWENYEWE
“Mimi na ndugu yangu tulikuwa tukiishi na baba na wadogo zangu wengine lakini baba alinihamishia mimi kwenye kitanda chake chumbani kwake nikawa nalala naye na akawa ananibaka usiku na asubuhi. Jua linapochomoza nilikuwa natoka,’’ alidai mtoto huyo.
“Nilikuwa naumia sana. Kila nilipoona usiku unaingia moyoni nilikuwa nikisema muda wa mateso umefika. Nilikuwa napenda kulala ili niamke kwenda shule, lakini baba alikuwa haniachii! Hali hiyo ilinifanya kesho yake nishinde nasinzia.”
ALIKUWA AKITUMIA VITISHO
Binti huyo aliongeza kuwa, pamoja na kuingiwa na akili ya kutaka kuwaambia majirani, lakini baba yake alimwendea mbele kama alijua kwani kila alipomaliza unyama huo alimwambia angemchoma kisu kama angetoboa siri hiyo kwa watu au kwa mama yake mzazi.
KUMBE MAMA ALIFUKUZWA
“Mtu wa kumwambia matatizo hayo ni mama yangu mzazi ambaye baba alimfukuza nyumbani na alikuwa akiishi sehemu nyingine. Hata hivyo, nilipomwambia mama kwamba baba anatubaka, hasa mimi usiku kucha mpaka naamka nimechoka na siwezi kutembea, aliniambia nisijaribu kumwambia mambo hayo ya kijinga.”
Binti huyo alitoa ya moyoni kuhusu kisa chake hicho cha kubakwa na kulawitia kwa kusema:
“Sijui ni nini?! Siku nyingine nikiwa na mdogo wangu tunayesoma naye shule, tuliitwa na babu mmoja anaitwa Elias. Tulikwenda hadi nyumbani kwake.
“Tulipofika, babu alitupa chipsi na kula. Halafu alimwambia mwenzangu atoke nje na kuanza kunibaka mimi. Alipomaliza, alimuita mwenzangu, naye akambaka. Alikuwa akitupatia chipsi kisha wakati wa kuondoka alitupa shilingi elfu mbili (2,000).
MARA TATU ZATAJWA
Uwazi lilipomuuliza binti mwingine wa miaka nane kuhusu kufanyiwa unyama huo, alisema: “Mimi babu Elias alinibaka mara tatu sehemu za mbele na sehemu za nyuma, akanipa shilingi elfu mbili na chipsi.”
MJUMBE WA MTAA AZUNGUMZA
Kwa upande wa balozi wa eneo hilo, Janet Tirisho alipoulizwa kuhusu ukatili huo, alisema kuwa alifanikiwa kuwaokoa watoto hao ambao walizoea kufanyiwa mchezo huo mchafu wa kubakwa kwa muda mrefu huku mama yao akidaiwa kupokea fedha kutoka kwa wanaye hao.Alisema sakata hilo walilifikisha Kituo Kikuu cha Polisi Arusha na watuhumiwa wakafunguliwa jalada lenye namba AR/RB/6252/2015- KOSA LA KUBAKA.
UCHUNGUZI WA KIDAKTARI
Daktari mmoja ambaye hakupenda jina lake kuandikwa gazetini alisema watoto hao wamefanyiwa uchunguzi na wamegundilika kuwa wameharibika vibaya sehemu zao za siri.
Naye Katibu wa Afya, Hospitali ya Mount Meru, Enjo Kimati, aliyezungumza kama msemaji wa hospitali hiyo alisema kuwa matukio ya ubakaji yameongezeka maradufu kwani watoto wenye umri wa miaka mitano hadi 15 wamekuwa wakifikishwa hosptalini hapo na kugundulika wamebakwa na kulawitiwa.
KAMANDA WA POLISI
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, SACP Leberatus Sabas (pichani) amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema: “Tumefanikiwa kumtia mbaroni babu Elias lakini baba mzazi, Emmanuel Ezekiel alitoroka. Jeshi la polisi linamsaka ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria kujibu shitaka la kubaka linalomkabili.”
VIA-GPL
No comments:
Post a Comment